
Akiongea na waandishi wa Habari,Katibu mkuu wa TFF Angetile Osiah amesema kitendo alichofanya Mwinyi Kazimoto kuondoka kambini bila Ruhusa ni kinyume cha maadili hivyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yake.
Katibu mkuu huyo amesema TFF haina sababu ya kumzuia mchezaji huyo ambaye inasemekana anakwenda kukipiga soka la kulipwa katika klabu mojawapo huko Qatar.
Katibu huyo amewataka wachezaji wengine ambao wanahitaji kwenda kufanya majaribio nje ya nchi kufuata taratibu wanapokuwa katika timu ya taifa badala ya kutoroka na kuanzisha hali ya sintofahamu.
Shirikisho hilo pia limekanusha uvumi uloenea kwamba limemzuia beki mahiri wa Simba Shomari Kapombe kutokwenda kufanya majaribio nchini Uholanzi na Afrika Kusini.
PICHA KWA HISANI YA MTANDAO
0 comments:
Post a Comment