Na Ali Issa Maelezo Zanzibar. 9/7/2013
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Fatma Abdull Habib Fereji amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Ofisi hiyo, Bodi ya madawa na vipodozi Zanzibar na Baraza la mazingira la Tanzania Bara kwa mashirikiano ya kufanikisha zoezi la kuangamiza unga mbovu uliokuwepo bandarini Zanzibar kuazia mwezi wa April mwaka uliopita hadi Julai mosi mwaka huu.
Pongezi hizo alizitoa leo huko Baraza la wakilishi wakati alipokuwa akitoa ufafanuzi juu ya hali halisi ya unga huo ambao haufai kwa matumizi ya binaadamu .
Amesema unga huo ulioharibika umeanza kuangamizwa kwa ushirikiano wa pande mbili za Muungano baaada ya Zanzibar kukosa eneo ambalo litaweza kuhifadhi afya za wananchi wakati wa kuuangamiza.
Amesema Serikali ya Muungano ilikubali ombi lao na kuanzia tarehe 14 Mei hadi tarehe 15 Juni kontena 15 za unga mbovu ulisafirishwa kupelekwa Tanzania Bara kwenda kuangamizwa.
“Tulizungumza na wezetu Tanzania Bara kutupatia eneo la kuteketeza unga huu tuna shukuru wezetu hawakutuvunja moyo walikubali na sasa umeshateketezwa chini ya usimamizi wa Baraza la Mazingiara ”, alisema Waziri huyo.
Aidha alifahamisha kuwa unga huo unateketezwa na kiwanda cha saruji cha Twiga simenti kilioko Tanga kwa makubaliano ya Wizara yake , Bodi ya madawa na vipodozi na msimamizi baraza la mazingira la Tanzania Bara.
Amesema kuanzia sasa hakutakuwa na muhali na vyakula vibovu vinavyo letwa na wafanya biashara na amewaomba wananchi washirikiane kufichua maovu hayo ili kulinda afya zao .
Unga huo unaofikia tani 780 uliingizwa nchini Aprili mwaka jana na Kampuni ya Bopary Inteprise kutoka nchini uturuki.
0 comments:
Post a Comment