Idara ya Uhamiaji hapa nchini inatrajia kukusanya kiasi cha zaidi ya Bilioni 85 kwa kipindi cha mwaka 2013/2014 ambapo makusanyo hayo yanatokana na mapato mbalimbali ya idara hiyo ambayo ipo chini ya Wizara ya mambo ya ndani.
Hayo yameelezwa na Kamishana wa utawala na fedha katika idara hiyo ambaye ni Bw Piniel Mgonja wakati akiongea katika mkutano wa tathimini wa utendaji kazi kwa wahasibu wa idara wa uhamiaji unaondelea Jijini hapa
Piniel alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kinaweza kupatikana na kuvuka malengo kutokana na ukusanyaji wa Madhuhuli kuboreshwa zaidi tofauti na miaka ya nyuma hali ambayo mpaka sasa itasaidia sana kuongezeka kwa mapato ya idara hiyo.
Mbali na hayo alisema kuwa hata kwa sasa vipo baadhi ya vyanzo vingine ambavyo navyo vimechangia sana kuongeza mapato katika idara hiyo ambapo vyanzo hivyo ni pamoja vyanzo vya vibali vya kuishi Nchini, huduma za Pasipoti, Hati za kusafiria,huduma ya uraia ,Viza kwa wageni wanaoishi hapa Nchini
Kutokana na hali hiyo alisema kuwa bado idara ya uhamiaji hapa nchini inakabiliwa na changamoto kubwa ambayo ni ukosefu wa huduma za kibenki katika baadhi ya vituo vya uhamiaji hapa nchini hali ambayo wakati mwingine inasababisha upotevu na umanifu wa kifedha kwa
wafanyakazi pamoja na wadau wa uhamiaji.
wafanyakazi pamoja na wadau wa uhamiaji.
Alisema kuwa hali hiyo si nzuri sana kwani nayo inachangia sana kupunguza hata mapato ya Serikali kwani baadhi ya mapato huwa
yanapungua au kupotea kabisa kutokana na ukosefu wa huduma za kibenki.
yanapungua au kupotea kabisa kutokana na ukosefu wa huduma za kibenki.
Awali Akifungua mkutano huo Katibu Mkuu wa wizara ya mambo ya ndani Nchi, bw Mbarak Abdulwakil alisema kuwa wahasibu katika wizara hiyo wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,Kanuni , na taratibu zilizopo kwani usimamizi wa fedha unataka usimamizi wa hali ya juu sana kwani fedha zinaushawishi mwingi sana
0 comments:
Post a Comment