Saturday, July 27, 2013

045Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Bi. Joyce Mkinga akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na utekelezaji wa dira ya Taifa ya Maendeleo hadi kufikia 2025 wakati wa mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar Es salaam kushoto ni Afisa Habari toka Idara ya Habari Bi. Fatma Salum.
PICHA ZOTE NA FRANK MVUNGI-MAELEZO
………………….
Na Georgina Misama-MAELEZO
Jumla ya shilingi trilioni 44.5 za kitanzania zinatarajiwa kutumika katika utekelezaji wa mpango wa maendeleo wa miaka mitano, ambapo Tanzania imedhamiria kufikia hadhi ya nchi zenye kipato cha kati na kuondokana na umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2025.
 
Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa kitengo cha mawasiliano, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango Joyce Mkinga alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo.
 
Joyce alitaja malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo, ambapo alisema katika miaka mitano ya kwanza vipaumbele vipo katika makundi ya Miundombinu ambayo inahusisha nishati, usafirishaji, TEHAMA, maji safi na maji taka na umwagiliaji, Kilimo ikijumuisha mazao ya chakula na biashara,Viwanda, Rasilimali watu na uendeshaji wa huduma za utalii, Biashara na fedha ni miongoni mwa vipaumbele vitano vya Taifa ambavyo serikali inatarajia kutekeleza.
 
“Mkazo mkubwa unatiliwa katika miradi ya maendeleo, tunaamini miradi ikiendelea vizuri, umasini utapungua. Tume ya mipango ina wajibu wa kufatilia miradi iliyowekewa kipaumbele na utekelezaji wake” alisema Joyce Mkinga.
 
Aidha Bi. Joyce alisema  kuwa  ili kufikia malengo jumla ya shilingi tirioni 8.9 zinahitajika kwa mwaka na kuongeza kuwa Serikali inakadiria kuwekeza kiasi cha wastani wa takriban shilingi trilioni 2.9, kwa mwaka wakati wastani wa shilingi trilioni 6.0 kwa mwaka zinatarajiwa kutokana na uwekezaji binafsi au ubia.
 
Itakumbuwa kuwa mpango wa matoke sasa ambao ulizundiliwa ambao ulizundiliwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mpango huu umelenga kuhakikisha utekekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 inafiiwa ifikapo mwaka 2025.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video