Tuesday, July 16, 2013


Na Baraka Mpenja
,“Safari bado ipo, sio muda muafaka wa kutafakari yaliyopita, tuangalie mbele katika mchezo wa Marudiano. Kama Uganda walitufunga Nyumbani, kwanini sisi tusiwafunge kwao?. Tulipata nafasi hatukutumia, wao wakapata moja wakatumia, lakini ndio soka na unatakiwa kukubali”. Haya ni maneno ya kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars baada ya kulala kwa bao 1-0 dhidi ya Uganda The Cranes uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wanandinga wa Taifa Stars wanaendelea kujifua katika dimba la CCM Kirumba , jijini Mwanza wakijiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda The Cranes kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani, CHAN, zitakazofanyika mwakani Bondeni, Afrika Kusini.
MMG27292Stars wanajifua kwa malengo ya kufuta kipigo cha bao 1-0 walichopata katika dimba la nyumbani na wana kibarua kizito mbele ya Uganda ambao mara nyingi wamekuwa wakifanya vizuri sana wakiwa kwao dimba la Nelson Mandela, Namboole, jijini Kampala.
Kocha wa Kim Poulsen anatakiwa kuwanoa vijana wake ili kupata ushindi wa mabao 2-0 na kufuzu fainali za CHAN, lakini kazi kubwa ni kurekebisha ubutu wa safu ya ushmbuliaji inayoongozwa na mshambuliaji wa timu ya Azam FC, John Raphael Bocco “Adebayor” pamoja na “Anko” Mrisho Ngassa ambao mechi iliyopita walishindwa kubadili nafasi kadhaa walizopata kuwa magoli.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI, Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF, Boniface Wambura Mgoyo amesema kikosi cha Taifa stars kipo salama jijini Mwanza na wachezaji bado wana morali ya juu sana kuelekea mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda.
“Kwa maana ya Kambi inaendelea vizuri, timu ipo Mwanza na kocha anaendelea kuwanoa vijana. Morali ipo juu sana, tulifungwa mchezo wa kwanza nyumbani, watu wengi hatukutarajia kiwango kile kwa timu yetu, lakini tuache kuwaza yaliyopita bali tuangalie ya mbele”. Alisema Wambura.
Wambura alisema kikubwa ambacho Kocha Kim anakisema ni kuwa timu yake ina uwezo wa kupata matokeo nchini Uganda, kwani kama wao walipata ushindi hapa nyumbani, kwanini Taifa stars isipata kwao.
ACREINN
Afisa habari huyo alisema Kim ameamua kuweka kambi jijini Mwanza kwani hali ya hewa ya Mwanza inafanana nay a Kampala, hivyo vijana watazoea kucheza katika hali sawa na ya Uganda.
Pia alisema Uwanja wa CCM Kirumba unapatikana muda wote na kukidhi matakwa ya ratiba yake ya mazoezi kuliko Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambao kuna wakati unatumika katika shughuli nyingine na kuharibu mipango ya kocha.
Wambura alisema mashabiki wa soka wa Tanzania wasife moyo kwani bado safari ni ndefu, hivyo mi muhimu kuisapoti timu yao ya Taifa.
“Soka halikui kwa siku moja, ni muhimu sana kwa mashabiki kuwa wavumilivu, timu yetu ni changa bado  kocha ana mipango mingi mizuri sana kwa ajili ya soka la Tanzania”.
Taifa stars inatarajiwa kusafiri kwenda jijini Kampala nchini Uganda mnano Julai  24 mwaka huu.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video