Supa D akiwa kanda ya ziwa, jijini Mwanza Supa D akiwa na vifaa vyake vya kufundisha mchezo wa masumbwi
……………………..
KOCHA wa Kimataifa wa mchezo wa Masumbwi Nchini, Rajabu Mhamila ‘Super D’ yupo katika ziara ya kutembelea mikoa mbalimbali hapa nchini tangia mwishoni mwa mwezi uliopita ambapo mpaka sasa katika ziara yake hiyo kasha tembelea mikoa kadhaa ya Tanzania Bara akianzia na Tanga, Moshi, Arusha, Karatu, Babati, Mwanza , Shinyanga na Kahama
Ziara hiyo yenye lengo la kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa vijana na kuwapa mbinu mpya baadhi ya makocha wa mikoa husika ili mchezo wa ngumi uweze kusonga mbele ingawa mchezo huo unapendwa na wenga na kukwepwa na wadhamini ndicho kitu kinachokifanya mchezo wa masumbwi uonekane umeshuka hadhi yake wakati bado upo juu
Akizungumzia safari hiyo Super D ” Amesema safari hiyo ni ya manufaa sana kwa watu wa mikoani kwani bado mikoa mingi atatembelea kutoa elimu ya mchezo huo na kuhamasisha vijana wengi wajiunge na mchezo huo kwani yaweza kuwa ni ajira yao
Super D ambaye ni kocha wa kwanza kutoa mafunzo yake kwa njia ya DVD zilizochanganywa na clips mbalimbali, CD hizo zilizotengenezwa kwa umakini wa ali ya juu ambazo ni chachu kwa ajili ya kuvutia wapenzi na mashabiki mbalimbali kujua mchezo wa masumbi
DVD hizo kwa sasa zinapatikana katika makutano ya barabara ya Uhuru na Msimbazi au unaweza kuzipata jengo la Azam lililopo mtaa wa Msimbazi karibu na kituo cha Polisi Post Gelezani wasiliana na kocha kwa simu 0713406938 ili uweze kupata dvd hizo kwa ajili ya kujifunza zaidi mchezo huo
DVD zina mabondia wakari wanaotamba Duniani kama vile Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali na wengine wengi Super D aliongeza kuwa mikoa mingine atakayotembelea ni Tabora,Singida,Dodoma,Morogoro,Iringa,Mbeya na Songea
0 comments:
Post a Comment