Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji mwenye matukio wa klabu ya Liverpool, wekundu wa Anfield “Majogoo ya jiji” na timu ya taifa ya Uruguay ambaye mzimu wake bado unawasumbua Waghana baada ya kuwanyima bao la wazi katika fainali za kombe la dunia mwaka 2010 nchini Afrika kusini, Namzungumzia Luis Suarez, amesisitiza nia yake ya kutaka kuihama klabu yake hiyo katika majira haya ya joto ya usajili kwa sababu anataka kucheza michuano ya Ulaya na amechukia jinsi ambavyo vyombo vya England vikimuandika vibaya.
Kauli hiyo ya Suarez amefungua njia kwa bosi wa washika bunduki wa London, Mfaransa Arsene Wenger ambaye anahangaika kutafuta mshambuliaji mkali zaidi na alituma ofa ya pauni milioni 30, lakini Liverpool wakaitupilia mbali.
Muruguay huyo ameweka wazi mipango yake ya kuondoka Anfield, na amefurahisha na timu zaidi ya mbili kumhitaji, huku akifurahia zaidi nia ya Arsenal kutaka kumsajili.
Suarez ameongeza kuwa kwa sasa wakala wake ambaye ni kaka yake wa kocha wa Bayern Munich, Joseph Pep Guardiola ndiye mwamuzi wa maisha yake ya baadaye.
Taarifa hii imekuja siku chache baada ya mshambuliaji mwenzake wa timu ya taifa ya Uruguay na klabu ya Napoli na mwenye dili kubwa kwa sasa Edinson Cavani kukaririwa akisema Suarez anataka kuondoka Liverpool kwa sababu anataka kucheza timu itakayoshiriki michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Janga la ghafla: Luis Suarez ameweka wazi kuwa anataka kuihama Liverpool na kujiunga na wapinzani wa majogoo wa jiji, klabu ya Asernal
Anamtaka mpaka basi: Meneja wa Gunners Arsene Wenger ana mipango mizito ya kuwa na Suarez msimu ujao
‘Ni kitu kizuri kuhitajika na timu kama Arsenal. Rafiki zangu wananipigia na kuniuliza kama naenda Chelsea, lakini nabaki kucheka tu”. Suarez ameimbia Redio ya Uruguay ya Sport 809.
Suarez aliendelea kusema kuwa kuna sehemu zaidi ya moja ya kwenda. Kuna timu mbili au tatu zinazomhitaji na Liverpool wanatambua kuhusu hilo.
Amerudi kibaruani: Brendan Rodgers na kikosi cha Liverpool wamerudi katika mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu nchini England, lakini Suarez hayupo mpaka sasa, bado anakula bata
Mkanganyiko? Suarez kwa mara ya kwanza alitoa sababu ya kuandikwa vibaya na vyombo vya habari vya England kuwa ndio sababu ya yeye kutaka kuondoka Liverpool, sasa ameongeza sababu kuwa anataka kucheza UEFA
Vyombo vingi vya habari vya nchini England vilimponda sana Suarez kwa kitendo cha kumng`ata beki wa Chelsea Branislav Ivanovic
Msela wake: Lakini Edinson Cavani (kulia) amesema nyota mwenzake wa Uruguay anataka kuondoka Anfield ili kucheza Champions League
0 comments:
Post a Comment