Saturday, July 27, 2013

Na Baraka Mpenja 
Baada ya Timu ya Tanzania, Taifa Stars kupigwa mabao 3-1 na Uganda “The Cranes”  katika harakati za kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani, CHAN na kutolewa kwa mabao 4-1 kutokana na kipigo kingine cha nyumbani cha 1-0 wiki mbili zilizopita uwanja wa Taifa , makocha mbalimbali wamesema kuna haja ya kubadili mfumo wa soka la Tanzania na kujenga misingi ya soka la vijana.
377424_513119925367515_1991119591_nUganda “The Cranes” wamefuzu kucheza fainali za CHAN mwakani nchini Afrika kusini baada ya kuitoa Taifa Stars kwa jumla ya mabao 4-1. Mechi ya kwanza jijini Dar es salaam, Stars walilala bao moja kwa bila na leo hii wamekung`utwa 3-1
JULIO (1)Kocha msaidizi wa klabu ya Simba, Jamhuri Kiwhelu  “Julio” ambaye kwa sasa yupo jijini Tanga kujiandaa na mchezo wa kesho wa kirafiki dhidi ya wagosi wa Kaya alisema matokeo ya leo yamesikitisha sana kwani kila mtu alikuwa na matarajio ya kufanya vizuri.
“Kwa kweli nimeumia sana, sikutegemea Stars kfungwa namna hiyo, lakini ndio soka bwana”. Aliongea kwa Julio kwa masikitiko.
Kiwhelu aliongeza kuwa kuna haja ya kuwa wavumilivu kwa sasa, huku akimnukuu kocha kim aliyewahi kukaririwa akisema kuwa timu imepata mafanikio muda ambao sio maufaka kwani timu inatakiwa kujenga zaidi, kwa maana hiyo kocha apewe nafasi ya kutekeleza mipango yake.
Julio alisema licha ya kupoteza mchezo wa leo na kukosa nafasi ya kucheza fainali za CHAN, lakini anawapongeza vijana kwa kucheza soka zuri na kupambana.
Julio alimaliza kwa kusema kuwa soka halijengwi kwa siku moja, hivyo lazima uvumilivu utawale.
mkwasasKocha wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa “Masta” amesema kuna haja kubwa ya kufanya mabadiliko ya soka la Tanzania kwasababu Uganda wanacheza soka sawa na la Tanzania, isipokuwa wanatumia nguvu zaidi na kujituma kwa wakati wote..
Mkwasa alisema wachezaji wa Stars hawana mipango ya uwanjani, hawajui wakabe vipi na washambulie vipi, hivyo kuna haja ya wachezaji kujitambua na kuwekeza katika mazeozi na kuzingatia maelekezo ya kocha pamoja na nidhamu ya uwanjani.
Kocha huyo alisema wachezaji wanaonekana kutokujitambua, kwasababu waliripotiwa kupunguza morali baada ya kufungwa mechi ya kwanza, kitendo ambacho ni uchanga katika soka, lakini ni aina ya wachezaji ambao Tanzania inamiliki, cha msingi ni lazima mwalimu awafundishe namna ya kucheza soka hasa namna ya kukaba.
“Kila siku makosa ni yale yale, kuna mazoezi mengi ya kuwafundisha wachezai namna ya kucheza, kukaba na kushambulia, ni wakati Muafaka kwa mwalimu kuangalia upya namna ya kuwanoa wachezaji wake, la sivyo itakuwa ngumu sana kwa Tanzania kufika mbali zaidi”. Alisema Mkwasa.
100_1462
Naye kocha wa zamani wa mabingwa wa Tanzania, klabu ya African Sporsts ya Tanga na kwa sasa mjumbe wa kamati yaufundi  ya klabu ya Simba, John Wiliam “Del Piero” Muumini mkubwa wa soka la vijana alikiri kuwa Taifa stars ilizidiwa na Waganda na lazima watanzania watambue kuwa Uganda wana uwezo mkubwa zaidi.
Hata hivyo Piero alisema mchezo wa kwanza ndio ulikuwa muhimu kushinda, lakini Stars walishindwa kuitumia nafasi na leo hii Waganda wametumia nafasi zao huku wakionekana toka mwanzo wa mchezo kuwa na nia ya kutaka kwenda Afrika kusini mwakani.
Piero alisema watanzania wengi walikuwa wanategemea miujiza, lakini soka haliendi hivyo, kikubwa ni maandalizi.
Kocha huyo alisema makosa yaliyojitokeza leo ndio yaleyale, hivyo kuna haja kubwa ya kuwekeza upya katika soka la vijana kwani ndio msingi wa soka la nchini Yoyote.
Kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas dk78, Aggrey Morris, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo/Simon Msuva dk43, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, John Bocco ‘Adebayor’/Haroun Chanongo dk78, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.
The Cranes; Hassan Muwonge, Hassan Waswa, Nicolas Wadada, Habib Kavuma, Savio Kabugo, Richard Kasaga, Dennis Iguma, Said Kyeyune/Ntege Ivan dk62, Joseph Mpande/Simon Okwi dk 72, Frank Kalanda/Lawrence Nduga dk 89 na Brian Majwega

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video