Tuesday, July 9, 2013


8E9U9199
Spika wa Bunge la Jamhuriya Korea Kusini Mhe. KANG Chang-Hee anafanya ziara ya siku tatu hapa nchini kuanzia tarehe 8 hadi 10 Julai, 2013, kufuatia mwaliko wa Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne S. Makinda (Mb).
AkiwanchiniSpika KANG Chang Hee tayari amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.  Kesho tarehe 9 Julai 2013, Spika KANG atakutana na mwenyeji wake (Spika wa Bunge la Tanzania) katika Ukumbi wa Mikutano wa Spika na kufanya mkutano wenye lengo la  kuimarisha ushirikiano baina ya mabunge ya nchi zote mbili.
Spika KANG ameambatana na ujumbe wa watu ishirini na watano  (25) wakiwemo Waheshimiwa Wabunge, Wakurugenzi wa Ofisi ya Bunge la Korea, Maafisa pamoja na Waandishi wa Habari. Katika Mkutano wake na Spika wa Bunge la Tanzania utakafanyika saa 4:00 asubuhi vyombo vya habari vya hapa nchini vinakaribishwa kuhudhuria mazungumzo hayo. Hii ni mara ya kwanza ziara ya kibunge inafanyi kakati kangazi ya Maspika baina ya Tanzania na Korea Kusini.

Tarehe 10 Julai 2013, Spika KANG Chang-Hee atakutana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe(Mb) katika Hoteli ya  Serena Jijjini Dar es Salaam.
Imetolewa na Ofisiya Bunge,
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma na
Uhusiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam.
08 Julai 2013

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video