Tuesday, July 16, 2013


f345Ruvu-Shooting
Na Baraka Mpenja 
Maafande wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) wenye makazi yao Mabatini Mlandazi mkoani Pwani , Ruvu Shooting wameanza kambi yao kujiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajiwa kuanza kushika kasi mnamo Agosti 24 mwaka huu.
Akizungumza na MATUKIO DUNIANI, Afisa habari wa klabu hiyo, Masau Bwire amesema wameingia kambini ikiwa ni siku chache tangu wawape mapumziko mafupi wachezaji wao baada ya kumaliza kushiriki mashindano ya maadhimisho ya miaka 50 ya Jeshi la kujenga Taifa nchini Tanzania (JKT).
“Tumeanza kujinoa vikali baada ya mapumziko mafupi, lengo letu ni kuleta mapinduzi ya soka nchini Tanzania, hakika msimu ujao tutakuwepo katika kinyang`anyiro cha kuusaka ubingwa wa ligi kuu ambao  wanajangwani Dar Young Africans waliutwaa msimu uliopia”. Alisema Masau.
Masau alisema wapo katika morali nzuri ikizingatiwa wamesajili wachezaji wazuri ambao kocha wao Charles Boniface Mkwasa “Masta” alipendekeza katika ripoti yake.
“Unajua soka la Tanzania limekuwa kama la Simba na Yanga, wanapokezana ubingwa kama mbio za kupokezana vijiti, sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko na kuwapindua wafalme hawa wa ligi kuu soka Tanzania bara, lazima tupambane sana kutafuta ubingwa msimu ujao”. Alisema Masau.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa ligi ya Tanzania bara ina mambo mengi ya ajabu,hususani waamuzi ambao mara nyingi hushindwa kutafsiri sheria 17 za soka na kuzinyima ushindi baadhi ya timu.
“Sina hakika kama wanafanya makusudi kuzinyima baadhi ya timu ushindi, nakumbuka msimu uliopita tulikuwa tunaonewa sana na waamuzi katika mechi zetu, mara nyingi tulifanyiwa vibaya na waamuzi bila kujua ni makusudi au la, lakini kama kutakuwa na haki msimu ujao, hatutanii lazima tuwe mabingwa au kushika nafasi tatu za juu”. Alisema Masau.
Masau alitamba kuwa msimu uliopita Ruvu Shooting ilikuwa inaonesha soka la hali ya juu na timu zilikiri, lakini kilichokuwa kinawasumbua ni makosa madogo ya safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa inapoteza nafani nyingi sana za kufunga.
Kwa upande wa kocha wa klabu hiyo, Mkwasa, alikaririwa na mtandao huu akisema anajiandaa kushindana zaidi msimu ujao na kuwapa mafanikio makubwa wapiga kwata hao wanaotumia uwanja wa mabatini mjini Mlandizi mkoani Pwani.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video