Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji wa Manchester ambaye kwa sasa hajatulia klabuni hapo, baba wa watoto wawili, Wayne Mark Roonye huenda akafirikiria kwenda washika bunduki wa kaskazini mwa London, klabu ya Asernal endao ndoto yake ya kufanya kazi na kocha wa Chelsea, Jose Mourinho haitatimia.
Manchester United wanakataa kumuuza Rooney kwa wapinzani wao wakubwa wa kuwania ubingwa msimu ujao, lakini bado nyota huyo anataka kuondoka Old Trafford.
Ingawa Chelsea ni chuguo la kwanza kwa Rooney, mshambuliaji huyo raia wa England anaweza kwenda Arsenal endapo David Moyes na bodi ya timu hiyo watakataa ofa ya pili ya Jose Mourinho.
Anaondoka? Wayne Rooney anawindwa na klabu za Arsenal na Chelsea
Arsenal walianza harakati za kumtaka Roonye ambaye atafikisha miaka 28 mwaka huu wakati ule amepigwa benchi na Sir Alex Ferguson katika mechi muhimu ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Real Madrid mwezi machi mwaka huu.
Arsenal wameonesha kuwa wanaweza kumlipa Rooney mshahara mzuri. Kwa sasa nyota huyo analipwa pauni milioni mbili na elfu arobaini kwa wiki na amebakisha miaka miwili katika mkataba wake, lakini The Gunners watavunja rekodi ya klabu kwa kumlipa pauni lakini mbili kwa wiki na mkataba wa miaka mitano.
Lakini Chelsea bado wanaongoza mbio za kumsainisha Roonye baada ya kutuma ofa ya pauni milioni 23, na kuongeza2.5 wiki iliyopita.
Baada ya kupata majeruhi ya nyama za paja katika ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu, Rooney anaendelea na mazoezi mepesi katika uwanja wao wa Carrington, huku akiwa na matumani kuwa klabu hizo mbili zitakubaliana juu ya yeye kuihama United.
Mama watoto wa Rooney, Coleen anaonekana kukubaliana na mume wake na ameweka wazi kuwa anapenda kuishi jijini London na watoto wao.
Ushindani: Jose Mourinho na Arsene Wenger wote wanamhitaji Rooney kutoka United
Ana presha kubwa? David Moyes anaweza kumpoteza moja kati ya majembe ya United
Rooney alizungumza kwa njia ya simu na kocha Moyes pamoja na mkurugenzi mkuu Ed Woodward baada ya kutokea tofauti kati yao juu ya umuhimu wake klabuni hapo.
Chelsea wanajiandaa kuongeza mzigo ili kumnasa Rooney, na taarifa zilizopatikana ni kuwa wanaandaa pauni milioni 30.
Kama United watakaa kumuuza Chelsea, basi itakuwa habari njema kwa Asernal kabla ya kumalizika kwa muda wa dirisha la usajili.
0 comments:
Post a Comment