Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji
hatari wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Dos
Santos Aveiro Ronaldo amemaliza uvumi wa kurudi katika klabu yake ya
zamani ya Manchester United , baada ya leo hii kukomelea msumari wa moto
kwa kuendelea kusisitiza kuwa maisha yake ya baadaye bado yapo Santiago
Bernabeu.
Nyota
huyo raia wa Ureno anayeshikilia rekodi ya dunia kwa kuhamishwa kwa bei
ya juu zaidi ya pauni milioni 80 kutoka United kwenda Real Madrid mnamo
mwaka 2009, anatakiwa na klabu yake hiyo iliompa jina na kuwa Ronaldo
wa leo.
Lakini
nyota huyo alizungumza na gazeti la Hispania la AS katika mji wa Gala,
Monaco na kusema kuwa United ni timu ambayo ipo katika damu yake kwa
muda mrefu na kila mtu anajua hilo, ila maisha yake ya baadaye bado yapo
Real Madrid.
Bado yupo yupo kwanza: Akiongea mjini Monaco, Cristiano Ronaldo amesema maisha yake ya baadaye yapo Real Madrid
“Nikiwa
Madrid nataka kupata mataji ya La Liga, na Ligi ya mabingwa. Pia
ninatumaini nitafuzu kucheza fainali za kombe dunia nikiwa na kikosi
changu cha timu ya Taifa ya Ureno”. Alisema Ronaldo.
Mapema wiki hii , Ronaldo aliuambia mtandao wa Sky Sports:
‘Kiukweli naikumbuka sana ligi ya England, nilipokuwa kule kila mtu
alijua kuwa Manchester United ni timu iliyopo karibu na moyo wangu”.
Real
wanafanya kila jitihada ya kuhakikisha nyota huyo mwenye umri wa miaka
28 anasaini mkataba mpya, lakini United chini ya Mkurugenzi wake wa
klabu kwa sasa, Sir Alex Ferguson wana amini watamrudisha Old Trafford.
Kwa upande wa Ronaldo alisema bado anaendelea na maisha ya Hispania.
‘kwa
sasa maisha yangu yapo Hispania na ninafurahi kucheza ligi ya huku.
Maisha yangu yapo hapa, lakini maisha ya baadaye huwezi kujua. Nina
furaha, furaha, furaha kubwa sana kucheza ligi ya Hispania”. Alisema
Ronaldo.
Siku zilizotukuka: Ronaldo kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kurudi katika klabu yake ya zamani ya Manchester United
Aliondoka
na kuacha mkwanja wa mrefu: Ronaldo aliihama Manchester kwenda Real
Madrid mwaka 2009 ada iliyovunja rekodi ya dunia ya pauni milioni 80
0 comments:
Post a Comment