Tuesday, July 9, 2013


_DSC0674Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akikagua mfumo wa maji taka katika kiwanda cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro_DSC0678Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga akiangalia sehemu ya kuni/magogo yaliyokusanywa na kiwanda cha 21st Century Textile Mill mkoani Morogoro. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkuu wa Wilaya Morogoro Bw. Said Amanzi
_DSC0684Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga (kulia) akitoa maelezo ya kiutendaji kwa Bw. P.V.Singh, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha  Century Textile Mill mkoani Morogoro juu ya uharibifu mkubwa wa mazingira unaotokana na nishati ya kuni/magogo yanayotumiwa kiwandani hapo katika shughuli za uzalishaji. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bw. Joel Bendera na Mkururenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Eng. Bonaventure Baya
……………………………
Na Lulu Mussa, Afisa Habari, Ofisi ya Makamu wa Rais
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mheshimiwa Charles Kitwanga, hii leo amefanya ziara katika baadhi ya viwanda Mkoani Morogoro kujionea hali ya Mazingira ikiwa ni pamoja na kuangalia mfumo wa maji taka katika viwanda hivyo.
Katika ziara hiyo Naibu waziri Waziri ameagiza wamiliki wa Kiwanda cha 21st Century Textile Mill kuacha teknolojia ya sasa ambayo inatumia nishati ya miti kwa wingi.
Mheshimiwa Kitwanga ametoa agizo kwa Baraza la Taifa na Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kukaa na uongozi wa Kiwanda hicho kukubaliana kimsingi matumizi ya teknolojia mbadala ya undeshaji wa shughuli za uzalishaji katika kiwanda hicho mfano mafuta mazito, gesi na makaa ya mawe.
Sambamba na hilo Waziri Kitwanga amewataka wamiliki wa Kiwanda hicho kutekeleza mara moja makubaliano baina yao na NEMC juu hatua za haraka za kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa kutumia miti mingi katika uzalishaji wa kila siku katika kiwanda hicho vinginevyo hatua kali zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kukifungia kiwanda hicho kuendelea na shughuli za uzalishaji.
Aidha, kiwanda cha 21st Centuy pia kimepewa muda wa mwezi mmoja kukamilisha taratibu za ukaguzi wa Mazingira (Environmental Audit) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mheshimiwa Joel Bendera aliyeambatana na Mheshimiwa Kitwanga katika ziara hiyo ameagiza kusitishwa mara moja uingizwaji wa magogo katika kiwanda hicho na kuahidi kusimamia kikamilifu zoezi hilo.
Bw. P.V. Singh, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda hicho ameoimba Serikali kumpa muda wa mwaka mmoja ili aweze kubadilisha mfumo mzima wa uzalishaji unaotumia takriban tani Hamsini za kuni/magogo kwa siku.
Katika ziara ya leo Mheshimiwa Kitwanga ametembelea Kiwanda cha Ngozi, Kiwanda cha Maturubai na Kiwanda cha Nguo 21st Century vyote vya Mkoani Morogoro.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video