Tuesday, July 9, 2013



8E9U0932
MIZA KONA – MAELEZO ZANZIBAR  
Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi UVCCM umeamua kutumia wazee wa Chama dhidi ya wanasiasa wanaopotosha na kutaka kutikisa misingi ya Mapinduzi na Muuungano wa Tanganyika na Zanzibar .
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari huko Makao Makuu ya CCM Kisiwanduwi Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana UVCCM Shaka Hamdu Shaka amesema watatumia wazee hao, wanaowaita silaha nzito, katika kukabiliana na maadui na mashetani wanaotaka kutishia ustawi wa amani, utulivu na Umoja wa Kitaifa.
Amesema kuwa katika kuyaimarisha Mapinduzi na Muungano   vijana hao wameamua kuwatumia wazee ili kusafisha hali ya hewa inayochafuliwa na wapinga umoja na mshikamano.
Amewataja miongoni mwa wazee hao ni pamoja na Rais mstaafuu, Komandoo Dk Salmin Amour Juma, Mzee Hamid Ameir Ali, Mzee Ibrahim Amani, Abdulrazaq Simai Kwacha, Mzee Ali Khamis Jaribu na Mzee Ali Ameir.
“Tumedhamiria kufanya kazi bega kwa bega na viongzi hao wakisimama upande wa UVCCM  katika kukiamsha na kukielezea kizazi kipya wapi tulikotoka, mahali tulipo sasa na kule tunakoelekea”.alieleza Naibu katibu Shaka.
Aidha alifahamisha kuwa viongozi hao watawatanguliza mstari wa mbele katika mikutano yote ya  UVCCM ili kuamsha ari ya kufanikisha mapambano dhidi ya wale wanataka kuvunja umoja na mshikamano uliopo.
“UVCCM hatukubali kuona mafanikio yaliyopatikana chini ya serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar yanavurugwa na Viongozi wachache wenye hulka ya na tama namaslahi yao binafsi”, alisisitiza nd. Shaka
Akizungumzia uchumi, Katibu huyo amesema kuwa utalii ni nguzo kuu inayojenga uchumi wa Zanzibar ambao unachangia asilimia 25 katika pato la Taifa na kufanikiwa  kwake linahitaji kuwepo na mazingira ya utulivu na amani.
Amesema UVCCM inalaani vikali kwa kujitokeza maneno ya ubaguzi dhidi ya Upemba, Uunguja na Ubara  kwa kisingizio cha mjadala wa uundwaji wa katiba mpya na kuwataka wananchi kuendelea kuishi kwa maelewano, umoja na kudumisha mshikamano nchini.
Ameeeleza kuwa UVCCM imejipanga kuzifufua maskani za CCM, kuimarisha mashina na vijana katika nyanja za kisiasa, kiuchumi na kijamii.
Aidha amewataka wananchi wapewe nafasi ya kutoa maoni yao katika mchakato wa katiba unaoendelea badala ya kujitokeza mamluki wachache kutaka kuwasemea wazanzibari
“Katiba ni matakwa ya wananchi hivyo waachiwe watowe maoni yao bila ya shindikizo na kushawishiwa na kundi au chama chochote cha siasa”, alielzea katibu huyo.
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video