Kocha wa klabu mpya ya ligi kuu soka Tanzania bara, Mbeya City ya jijini Mbeya, itakayoaanza mitanange ya ligi kuu Agosti 24 uwanja wa nyumbani wa Sokoine dhidi ya Kagera Sugar, mwalimu Juma Mwambusi amesema vijana wake wanaendelea vizuri, wana mwitikio mkubwa wa mazoezi na programu yake inakwenda vizuri , huku akiweka wazi kuwa amewachanganya wachezaji wa zamani na wapya ambao wanaonekana kuelewana sana.
Mwambusi ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa muda bado upo na anafanya jitihada kubwa kukiandaa kikosi chache kwani ligi kuu ni ngumu na inahitaji ushirikiano mkubwa baina ya viongozi na makocha, wachezaji na makocha bila kusahau viongozi na wachezaji.
“Ligi kuu ni ngumu sana, TFF wameshapanga ratiba yao, mimi nikiwa kocha kazi yangu ni kuandaa kikosi, nawaomba mashabiki watuunge mkono kwani wao ni mchezaji wa 12 uwanjani. Kwasasa tunaendelea na mazeozi ya viungo kuweka sawa miili na hii ni wiki ya mwisho, baada ya hapa nitaangalia program nyingine”. Alisema Mwambusi.
Kocha huyo alisema mapema mwezi ujao wanaanza mechi za kirafiki kupima uwezo kikosi chao, lakini kwa sasa ratiba inaenda kama walivyopanga.
Jiji la Mbeya kwa sasa linawakilishwa na timu mbili ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao kwa maana ya Maafande wa Tanzania Prisons na Mbeya City.
Mbali na Mbeya City, timu nyingine mpya za ligi kuu ni Rhino Rangers ya mkoani Tabora na wauza mitumba wa Ashanti United ya jijini Dar es salaam.
0 comments:
Post a Comment