Na Baraka Mpenja
Mkali
wa mchezo wa ndondi ama ndonga nchini Tanzania “Simba Asiyefugika” ,
kipnezi cha mashabiki jiji Dar es salaam, Thomas Mashali ametamba
kumtandika vikali bondia kutoka nchini Kenya, Patrick Amote katika
pambano la mchezo huo litakalopigwa hapo kesho (Julai 7) uwanja wa Taifa
jijini Dar es saalam katika Tamasha la Matumaini ambalo mwaka huu ni
maalumu kwa kuchangia Elimu.
Mashali ameumabia mtandao wa MATUKIO DUNIANI kuwa
amefurahi kucheza na Mkenya katika Tamasha la kuchangia Elimu ambapo
mgeni rasmi atakuwa Rais wa Tanzania mheshimiwa DKT. Jakaya Kikwete,
hivyo amefanya maandalizi mazuri kuhakikisha anamshusha Amote ulingoni
kwa makonde ya maana.
“Elimu
ni muhimu sana, nimefurahi kuwepo katika tamasha hili maalumu, ili
kuhakikisha nawafurahisha mashabiki wangu, ninalazimika kumpiga Mkenya
na lazima nitafanya hivyo kutokana na maandalizi mazuri niliyofanya”.
Alisema Mashali.
Bondia
huyo mwenye uwezo wa juu kwa sasa amekiri kuwa Mkenya Amote ni moja
kati ya mabondia wazuri ukanda wa Afrika mashariki, hivyo ni lazima awe
makini akiwa ulingoni.
“Amote
anaujua mchezo, lakini mimi niko tayari kupambana naye, nimejipanga
kuwafurahisha Watanzania watakaokuwepo uwanjani kuchangia Elimu, kikubwa
Baba wa nchi atakuwepo, lazima aone shughuli ya mwanawe”. Alisema
Mashali.
Pia aliwataka mashabiki kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo la kihistoria kuwahi kutokea nchini Tanzania.
“Joto
la Tamasha la mwaka huu si mchezo, mambo ni ya ajabu yatakayofanyika,
tujumuike kwa wingi kuchangia Elimu, kwa pamoja tutafika”. Alisema
Mashali.
Miongoni
mwa burudani za aina yake zitakuwa ngumi za utangulizi ambapo
Mheshimiwa Zito Zuberi Kabwe atapanda ulingoni kutunishiana msuli na
Vicent Kigosi “Ray”, Mheshimiwa Halima Mdee atapigana na Jackline
Wolper, wakati Aunt Ezekiel atapambana na Mheshimiwa Ester Bulaya.
Burudani
ya muziki, msanii mkali wa Tanzania Nasib Abdul “Diamond” kipenzi cha
warembo atapambana jukwaani na mkali wa Kenya, Prezzo.
Katika
soka Wabunge mashabiki wa Simba na Yanga watashuka dimbani kuwania
kombe, na burudani ya aina yake ni kwamba, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, DKT. Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa mgeni rasm na
refa wa mechi hyo.
Hakika ni maMbo ya ajabu sana, “Presidaa” atachezesha mechi? Kwa pamoja Watanzania tujitokeze kwa wingi zaidi hapo kesho.
0 comments:
Post a Comment