Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United wamecheza mechi yao ya tano katika ziara yao ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi dhidi ya Kitchee ndani ya uwanja wa Hong Kong na kuibuka na ushindi wa mabao 5-2.
Mechi ya leo ilitakiwa kuchezwa mwishoni mwa wiki iliyopita, lakini Kocha wa United, David Moyes alilazimika kuahirisha mechi kwa madai kuwa uwanja wa Hong Kong ulikuwa mbovu kufuatia mvua kunyesha na uwanja kujaa matope, huku ukiwa umetumika mfululizo katika michuano ya kombe la Barclays la Asia.
Hali ya uwanja siku ya jumamosi wakati wa fainali ya Sunderland na Manchester City ilikuwa mbaya sana, lakini viongozi walijitahidi kufanya jitihada za kurekebisha kabla ya mchezo wa leo.
Kikosi cha Kitchee: Comi, Rodriguez, Rehman, Kei, Alkande, Belencoso, Wai, Annan, Yang, To.
Wachezaji wa akiba: Jianqiao, Wen, To, Fung, Quankun, Hau, Fai, Paramo, Lam, Deshuai, Lung
Waliofunga Magoli yao: Lam (53), Alkande (69)
Kikosi cha Manchester United: Amos, Evra (Buttner HT), Anderson, Smalling, Carrick (Jones 72), Young (Januzaj HT), Welbeck (Lingard HT), Fabio (Rafael 72), Cleverley, Zaha, Keane.
Wachezaji wa Akiba: Lindegaard, Rafael, Jones, Ferdinand, Giggs, Van Persie, Buttner, Lingard, Januzaj.
Waliofunga mabao: Welbeck (16), Smalling (22), Fabio (26), Januzaj (47), Lingard (80)
Mashabiki wapatao 40,000-walijitokeza uwanja wa Hong Kong kuitazaman mechi hiyo
Safi kijana: Tom Cleverley na Anderson wakimpongeza Fabio baada ya kuifungia United bao la tatu
Risasi: Lam Ka Wai (wa pili kulia) akishangilia bao la kwanza la kusawazisha na kufanya ubao wa matangazo kusomeka 4-1
Bao la kwanza: Danny Welbeck akishangila bao lake la kwanza katika ushindi wa leo
Hapa rangi nyekundu tu: Uwanja wa Hong Kong ulijaza mashabiki wengi ambao lengo lao lilikuwa kuwashuhudia wakali wa soka la England
0 comments:
Post a Comment