Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa Manchester United, David Moyes huenda akapata pigo lingine baada ya kiungo wa FC Barcelona, Cesc Fabregas kumwambia kocha wake Tito Vilanova kuwa anataka kubakia kwa wazee wa Katalunya.
Jana, United walithibitisha kutuma ofa ya pauni milioni 26 ili kumsajili Febregas, nahodha wa zamani wa washika bunduki wa kaskazini mwa London, klabu ya Asernal.
Dili la kumhitaji Febregas limekuja baada ya Thiago Alcantara kujiunga na kocha wake wa zamani Pep Guardiola katika klabu ya Bayern Munich badala ya kujiunga ma mabingwa wa ligi kuu soka nchini England, Manchester United.
Mambo yamekuwa magumu kwa United baada ya kocha wa Barca Tito Vilanova kuweka wazi kuwa amezungumza na Febregas ambaye amesema anataka kubakia Camp Nou.
Vilanova alisema: ‘Cesc amepokea ofa kutoka klabu nyingine. Nilizungumza naye na ameniambia anataka kubakia hapa. Ndoto yake ni kutwaa makombe hapa”
“Tunafurahi kuwa na Cesc. Nafahamu amepata ofa nyingi, lakini ameniambia kuwa, ana furaja ya kuwepo Barca, hakuna haja ya kuondoka.’





0 comments:
Post a Comment