Tuesday, July 9, 2013


SONY DSCIMG_0399Kiungo mwenye uwezo wa kupiga pasi na kuchezesha timu, Haruna Moshi “Boban” (Juu) na beki nguli wa kati Juma Nyoso (chini) wote wawili walisimamishwa na wekundu wa Msimbazi Simba kwa tuhuma za utovu wa nidhamu, lakini Wagosi wa Kaya wamewasajili kwa ajili msimu mpya wa ligi kuu Tanzania bara unaotarajiwa kuanza kushika kasi Agosti 24 mwaka huu
IMG_8976
Na Baraka Mpenja 
“Siku hazigandi, aliimba mwanamuziki maarufu Lady Jaydee kwa sasa akijiita Anaconda”.
Hivi ndivyo unavyoweza kusema baada ya timu nyingi za ligi kuu soka Tanzania bara kuanza maandalizi ya msimu mpya wa ligi hiyo unaotarajia kufunguliwa Agosti ya 24 mwaka huu.
Kwa hesabu za haraka haraka umebaki mwezi mmoja tu ili viwanja vianze kuhimili daluga za wanaume 22 watakaotandaza kandanda kila mechi ya ligi hiyo.
Wakati maandalizi yakianza kushika kasi, Wagosi wa kaya, Wagosi wa ndima,  Coastal Unioni ya jijini Tanga, “waja leo waondoka leo”, , mabingwa wa mwaka 1988, wameanza mazoezi yao jana na kupiga jalamba la nguvu huku wakijivunia makombora yao mapya waliyoyasajili mpaka sasa.
Afisa habari wa klabu hiyo, Edo Kumwembe akizungumza na MATUKIO DUNIANI ametamba kuwa msimu ujao klabu hiyo imejipanga kutwaa taji ambalo linamilikiwa na wanajangwani kwa sasa.
“Mazoezi yameanza leo (jana) rasmi mkoani Tanga, wachezaji wengi wamewasili wakati wengi wanatarajiwa kuwasili hivi karibuni, nia yetu ni kuleta ushindani mkubwa sana na kushinda taji la ligi kuu. Na ndio maana tumefanya usajili wa wachezaji wazuri wenye viwango bora”. Alisema Kumwembe.
Kumwembe alisisitiza kuwa kutokana na usajili wao makini ambapo wamenasa baadhi ya mashine kama beki nguli kutoka kwa Wekundu wa Msimbazi Simba, Juma Said Nyoso, Kiungo fundi, mdogo wake Idd Moshi Mnyamwezi, namzungumzia Haruna Moshi Shaban “Boban” kutoka Simba, kiungo wa timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars ya Kenya, Chrispin Odula anayeungana na Mkenya mwenzake, kiungo wa zamani wa Simba, Fundi Jerry Santo, hakika watatwaa ndoo ya ligi kuu kama walivyofanya mwaka 1988.
“Msimu uliopita hatukufanya vibaya sana wala vizuri sana, haikuwa malengo yetu hata kidogo, sisi tulikuwa tunahitaji kuchukua ubingwa au kushika nafasi tatu za juu, kocha wetu Hemed Morroco alijitahidi sana, lakini mambo yalienda mrama, kwa msimu ujao tupo kamili gado”. Alisema Kumwembe.
Wakati Kumwembe akimwaga sera za Wagosi wa Kaya, mazoezi ya jana, kocha wao mkuu ambaye aliwahi kuwa kocha timu ya taifa ya Zanzibar, Hemed Morroco hakuhudhuria wakati wanandinga wake wakipasha moto misuli.
Morroco alizungumza na MATUKIO DUNIANI na kueleza kuwa jana jioni alikuwa safarini kuelekea Mkoani Tanga tayari kwa kujiunga na vijana wake wa kazi leo hii.
“Hivi tunavyozungumza nipo njiani kuelekea mkoani Tanga, mazoezi yameanza leo (jana), kikubwa tunajipanga vizuri zaidi.
Hivi karibuni viongozi wa Coastal Union chini ya Mkurugenzi wao wa Ufundi , Bin Slum walisema wanataka kuboresha mazingira mazuri kwa wachezaji wao kwa kuwapangia hoteli nzuri ili wafikirie soka tu na si vinginevyo na akiwezekana kujenga makazi yao ya kudumu ambapo wasaka kabumbu wao watakaa kwa raha zote na kula bata huku wakipigwa na viyoyozi kila kona.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video