Na Baraka Mpenja
Wakati
mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Dar Young Africans
wakitarajiwa kushuka dimbani leo hii kupambana na mabingwa wa Uganda,
KCC FC katika uwanja wa CCM Kirumba mkoani Mwanza, nao watani wao wa
jadi “Taifa kubwa” , Wekundu wa Msimbazi Simba wapo njiani kuelekea
mkoani Tabora ambapo wana ziara ya mikoani kama Yanga waliopo kanda ya
ziwa.
Yanga katika ziara hiyo, watacheza mechi
tatu za kirafiki na baada ya leo, itarudiana na KCC Jumapili Uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga kabla ya Alhamisi kukamilisha ziara yake kwa
kucheza na maafande wa Rhino Rangers FC, mjini Tabora Uwanja wa Ally
Hassan Mwinyi.
Akiwa
njiani katika basi lao, Mazungumzo yangu na Kocha wa Simba, Abdallah
Kibadeni, “King Mputa” mchana huu yamekwenda kama ifuatavyo:
Mpenja: Kibadeni habari yako?
Mpenja: Nzuri ndugu yangu, vipi za kwako?
Mpenja: Mimi mzima wa afya.
Kibadeni: Jambo la kheri hilo, ni muhimu kumshukuru Mungu.
Mpenja: Vipi maeneo ya wapi muda huu?
Kibadeni: Nipo Dodoma kwa sasa.
Mpenja: Waenda wapi Mputa?
Kibadeni: Niko na timu yangu tunaeleka Tabora.
Mpenja: Kufanya nini Tabora?
Kibadeni: Tuna ziara ya mikoani ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu mpya.
Mpenja: Vipi ukifika huko programu yako ikoje?
Kibdeni:
Nina mipango ya kucheza mechi za kirafiki ikiwa ni sehemu ya kupima
uwezo kikosi changu. Unajua ninajipanga vizuri sana kuhakikisha nachukua
kombe msimu ujao, nimesajili kikosi kizuri na kila kitu kipo sawa.
Mpenja: Kikosi chako kwa asilimia kubwa kimejengwa na vijana wadogo, unaamini watakusaidia?
Kibadeni:
Ndiyo! Kwanza kumbuka kikosi hiki kwa asilimia kubwa ndicho
kilichomalizia ligi kuu msimu uliopita. Mimi binafsi ni muumini mkubwa
wa soka la vijana, nadhani wana uwezo mkubwa sana, nimewapima mara
nyingi pale Kinesi na wanaonekana kuwa bora zaidi.
Mpenja: Msimu uliopita utovu wa nidhamu ulitwala Msimbazi, vipi umejipangaje msimu ujao?
Kibadeni:
Nimejipanga vizuri sana, na ndio maana aina ya wachezaji tulionao kwa
sasa wana nidhamu ya hali ya juu, mtovu wa nidhamu haji kupata nafasi ya
kucheza katika kikosi changu. Tumesajili wachezaji bora na wenye
nidhamu kubwa.
Mpenja: Unawaambia nini mashabiki wa Simba?
Kibadeni:
Timu yao ni nzuri, watuombee dua njema ili kila kitu kiende sawa,
mipango si matumizi, unaweza kupanga hilo mambo yakaenda mrama, lakini
sisi tuko makini kuanzia usajili na mazoezi kwa ujumla, hivyo watuunge
mkono muda huu mpaka tutakapomaliza ligi.
Mpenja: Basi ukifika Tabora tutawasiliana.
Kibadeni: Sawa , kila la heri na kazi njema ndugu yangu. Karibu sana.
Mpenja: Asante! Safari njema na mfike salama salimini.
Kibadeni: Inshallah.
Msomjai wa Mtandao huu , Kibadeni akifika huko Tabora tutaongea naye kama kawaida na kupata habari za huko.
0 comments:
Post a Comment