Mwenyekiti
wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba akiongea
na waandishi wa Habari (hawamo pichani) jijini Dar es Salaam leo, kuhusu
kuundwa kwa mikutano ya mabaraza ya katiba yanayotarajia kuanza kufanya
kazi Julai 12, 2013. Mwenyekiti
wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Mstaafu Joseph Warioba akiongea
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, kuhusu mikutano ya
mabaraza ya Katiba inayotarajiwa kuanza Julai 12 mwaka huu kwa ajili ya
kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Rasimu ya katiba ilitolewa 3 Juni
2013.Kulia ni Katibu wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Assaa Rashid.
(Picha zote na Lorietha Laurence Maelezo)
……………………………………………………………
Na Belinda Kweka- MAELEZO
TUME
ya Mabadiliko ya Katiba imeandaa mfumo wa uendeshaji wa mikutano ya
Mabaraza kuanzia Julai 12 hadi 2 Agosti mwaka huu, ambao utatoa ushiriki
mpana kwa kila mjumbe kuchangia na kutoa mawazo yake kwa uhuru na
uwazi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema mkutano hiyo
ni ya kujadili na kutoa hoja za msingi kwa maslahi ya Taifa na si kupiga
kura au kutetea maslahi ya kundi au watu fulani.
Jaji
Mstaafu Warioba alisema wajumbe wa mabaraza hayo hao wa mabaraza
kushiriki na kutoa mawazo yao kwa uhuru bila kuingiliwa na taasisi au
mtu yoyote ili kupata Katiba yenye maslahi na taifa.
“Napenda
kuwahakikishia Watanzania kuwa kila mjumbe atapata fursa ya kushiriki
kwa kutoa maoni bila ya kuingiliwa na mtu yoyote kwa kuzingatia taratibu
ambazo zitawekwa na Tume katika kuendesha na kusimamia mikutano hiyo”
alisema Jaji Mstaafu Warioba.
Aliongeza
kuwa Wajumbe wa Mabaraza takribani 20,000 wamepata Rasimu hiyo ya
katiba pamoja na mashirika, ambapo alisema Tume hiyo imepanga kuanzia
julai 12 mwaka huu itaanza kugawa Rasimu hiyo katika kila kijiji ili
kuweza kuifikia nchi nzima.
Pia
amesema Tume itatumia siku 54 katika kuendesha mabaraza ya katiba ya
wilaya kwa nchi nzima na imejigawa katika makundi 14 na kila kundi
litaendesha mikutano hiyo katika mamlaka za Serikali za mitaa 12 au 13.
Jaji
Warioba pia alifafanua kuhusu hoja ya Serikali tatu na kusema kwamba
hayo ni maoni yalitolewa na wananchi wenyewe na si yeye binafsi na suala
hilo lipo takribani miaka 30 nchini hivyo si geni kwa Serikali.
0 comments:
Post a Comment