KLABU
ya Arsenal sasa inakabiliwa mpambano mkali ili kumnasa Gonzalo Higuain
kutoka Real Madrid, baada ya taarifa nchini Hispania kusema kwamba
vigogo hao wa Hispania watataka ada kubwa ya uhamisho wa nyota huyo wa
Argentina.
Licha ya tetesi kuenea kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 yuko njiani kutua Kaskazini mwa London, gazeti la Marca limesema
hakukuwa na makubaliano baina ya klabu hizo mbili, maana yake zoezi la
muda mrefu la uhamisho wa nyota hiyo linaendelea.
Tayari au hapana? Sakata la Higuain kuhamia Arsenal bado bichi
Kuwasili
kwa Carlo Ancelotti kama kocha wa Real kulifikiriwa kungefungua milango
ya uhamisho huo, lakini gazeti la Hispania limesema Higuain zaidi
anaweza akabaki Bernabeu.
Bei
ya Pauni Milioni 23 iliyotajwa, inafikiriwa ni uzushi kwani vigogo hao
wa Hispania hawajataja bei rasmi ya kumuuza mwanasoka huyo wa kimataifa
wa Argentina, ambayo inaweza kuwa pigo kwa Arsene Wenger.
Baba
yake Higuain alisema mapema wiki hii kwamba uhamisho huo unaweza
kukamilika muda si mrefu, lakini taarifa za Hispania zinasema Real
inaweza kuamua kubaki na mshambuliaji huyo.
0 comments:
Post a Comment