Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Waziri wa Afya Zanzibar Juma Duni Haji amesema ili kuondokana na kutokuwa na uhakika wa upatikanaji wa dawa za kutosha katika Hospitali za Serikali hapa nchini , Wizara ya Afya imekubaliana na shirika la maendeleo la Den Mark (Danida) kuanzisha mfuko maalum wa dawa muhimu ambao utaruhusu washirika wengine wa maendeleo kuweza kujiunga na mfuko huo.
Amesema mfuko huo utakua na akaunti maalumu ambayo itafunguliwa baadae kwa ajili ya ununuzi wa dawa hizo.
Hayo ameyasema leo huko Baraza la Wakilishi mbweni nje kidogo ya mji wa zanzbar wakati alipo kuwa akisoma Bajeti ya makadirio na matumizi ya fedha ya wizara hiyo kwa mwaka 2013-2014 mwaka wafedha .
Amesema katika kutimiza azima hiyo shirika la Danida limekubali kuchangia shilingi za kitanzania bilioni mbili kuazisha mfuko huo na Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imetakiwa kuchangia shilingi milioni miatano fedha ambazo ni kwaajili ya dawa muhimu kwa vituo ya vijijini ,hospitali za wilaya ,na hospitali ya rufaa ya Mnazi Moja
Amesema katika utaratibu wa ununuzi wa dawa kutoka mfuko huo tayari kuna mtalamu elekezi kusaidiana na watalamu waliopo ili kufanikisha azma hio .
“upo utaratibu maalumu uliopanngwa wa kuzinunua dawa hizi muhim‘Framework Contract ‘utatumika kutoka mfuko wa dawa”.alisema Duni.
Aidha alisema kua kwa upande wa dawa za ziada ambazo zinatumika zaidi katika Hospitali na vituo vyake vya afya hapa nchini zitanunuliwa kwa kutumia bajeti ya serikali ya bilioni 1.5 ambazo ni kati ya bilioni 2.1 zilizo tengwa kwa ajili ya ununuzi wa dawa kwa mwaka huu wa fedha .
Hata hivyo waziri huyo ali sema wizara imepata mafanikio makubwa katika utendaji katika shughuli zake zakilasiku kwa kupunguza vifo vya kina mama na watoto kutoka 284.7kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2011 kufikia 221 kwa kila vizazi hai 100,000 mwaka 2012 uliopita.
Alisema wizara imeazisha chanjo mpya ya ‘rotvirus ‘ dhidi ya maradhi ya kuharisha ,uti wa mgongo na kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi makundi maalumu kama vile wanaume wanao jamiana kutoka 12.3%mwaka 2008 na kufikia 2.6%mwaka 2012 na watumiaji wa madawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindno kutoka 16% mwaka 2008 hadi 11.3% mwaka 2012 mwaka uliopita .
Wizara hiyo kwa mwaka huu wa fedha 2013 hadi 2014 ime pangiwa kuchangia jumla ya Tsh . 924,000,000 kwenye mfuko mkuu wa Serikali na kutumia Tsh .5,764,000,000 kwa kazi za kawaida ,Tsh 1,368,000,000 ikiwa ni ruzuku na Tsh 14,186,000,000 kwa mishahara na maposho.
kwa kazi za maendeleo wizara imepangiwa kutumia jumla ya Tsh 6,333,000,000 kutoka mfuko mkuu wa Serikali ,Tsh 37,257,128,000 misaada na Tsh .5,078,489,000 ikiwa ni mikopo kutoka nje .
Wakati huohuo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema jumla ya wanafunzi watano na mahabusu saba wa chuo cha mafunzo Zanzibar wamepatiwa haki ya kutoa maoni yao katika mchakato wa kuandaa katiba mpya ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hayo yamesemwa leo huko Baraza la wakilishi Zanzibar na Waziri wa nchi afisi ya Rais na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu suali la Jaku Hashim Ayoub alietaka kujua wafungwa wangapi na mahabusu Zanzibar ambao walipata haki ya kutoa maoni kuhusu mabadiliko ya katiba mpya ya jamuhuri ya Muungano Tanazania .
Amesema hali hiyo ilifanywa kuwapa nafasi watu hao kwa kuzingatia haki za binaadamu na sio jina la mazingira ya watu hao waliko .
Ali sema serikali huwa inatoa ruhusa malumu pale inapo tokea haja ya wanafunzi na mahabusu kutoa maoni kwa mujibu wa katiba hupewa frusa hiyo.
“Serikali ilipokea maombi kutoka tume ya mabadiliko ya Katiba ya kutaka kupokea maoni kutoka kwa wanafunzi na Mahabusu waliopo katika vyuo vya mafunzo vilioko kisiwani pemba maombi hayo yalikubaliwa na wanafunzi na mahabusu walipata frusa ya kutoa maoni yao” alisema Mwinyihaji.
Amesema serikali iliwajibika kuwapa frusa watu hao kwani nao ni sehemu ya jamii na binaadamu bali wamehitalifiana kwa baadhi ya mambo na makosa walio fanya .
Aidha alisema frusa ya kuwasiliana baina ya wanafunzi au mahabusu na jamaa zao na watu wengine ,sheria za chuo cha Mafunzo ni kuandika Barua ambazo hutumwa kwa ndugu na jamaa na ile ya kuonana uso kwa uso na watu ambao yeye mwenyewe amewaomba kuwaona frusa hiyo ipo na haina pingamizi .
0 comments:
Post a Comment