Mkurungenzi wa makosa ya jinai wa jeshi la polisi nchini Tanzania DCI ROBERT
MANUMBA amewashukuru wananchi kwa kuonesha utulivu na amani
wakati wa ziara ya Rais Baraka Obama hapa nchini amesma hayo mwakati
akizungumza na wandishi wa habari makao makuu ya jeshi la polisi jijini
Dar es salaam leo
Aidha katika mkutano huo na
waandishi wa habari Manumba amesema pia jeshi la polisi nchini
limefanikiwa kukamata meno ya tembo mia tatu na arobaini na moja
maeneo ya kimala jijini dsm baada ya jeshi la polisi kufanya upelelezi
dhidi ya majangili wa tembo hapa nchini
Pia katika taarifa yake kwa
waandishi wa wahabari dci manumba ameeleza pia kuwa jeshi la polisi
linamshikili raia mmoja wa uingereza kwa tuhuma za kigaidi hapa nchini
mala baada ya jeshi lapolisi kumkamata mtu huyo akiwa katika safari
mpaka wa kuvuka kwenda nchini Malawi toka nchini Tanzania,
Manumba amefanuna kwamba
mtuhuyo alikutwa na pasi mbili za kusafilia za Tanzania na Uingereza
ambazo sio harari na zimebainika kuwa nimiongoni mwa pasi zilizo potea
katika idara ya uamiaji hapa nchini.
Pia Dci amesema mala baada ya
jeshi la polisi kupeleleza limebaini kuwa mtu huyo ni raia wa
uingereza na alikuwa akitafutwa na serikali ya uingereza kwa tuhuma
mbalimbali za kigaidi mtuhuyo mwenye asili ya kiarabu na anauraia wa
Tanzania na uingereza. pia munumba amemewahadhalisha wananchi dhidi ya
vitendo vya kigaidi na kusema kuwa bado vikundi vya kigaidi vipo na
vinafanya matukio ya kihalifu hapa nchini na AFRIKA MASHARIKI NA DUNIA
NZIMA Pia alitaja mitandao hiyo kuwa ni mtandao wa alshaababu ,
bokoharamu na alquider kuwa vikundi hivyo bado nihatari kwa taifa letu
na afrika mashariki na dunia nzima kwa ujumla wake.
0 comments:
Post a Comment