Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Kocha wa Chelsea atarudi na furaha nchini England baada ya klabu yake ya Chelsea kumaliza ziara yake barani Asia kwa kuifungwa timu ya mastaa wa Indonesia ”Indonesia All-stars” mabao 8-1, lakini kikubwa zaidi kwake ni jinsi wachezaji wake vijana walivyoonesha kiwango cha juu na morali ya kufanya kazi naye.
Romelu Lukaku amedhihirisha utata wake wa kufumani nyavu baada ya kufunga mabao manne ndani ya dakika 134 na mchezaji aliyeko katika majaribio Chelsea ameonesha uwezo baada ya kufunga bao leo katika dakika ya 50, hivyo kuendelea kujiwekea mazingira ya kusajliliwa na Mourinho.
Kevin De Bruyne alicheza kwa kiwango cha juu wakiwa Bangkok na Kuala Lumpur, pia Nathaniel Chalobah alionesha kiwango kikubwa sana mjini Jakarta
Kikosi cha Chelsea leo: Blackman (Schwarzer 46); Wallace (Ivanovic 46), Cahill, Terry (Kalas 46), Bertrand (Cole 46); Chalobah (Essien 46), Van Ginkel (McEachran 60); Ramires (Feruz 60), Hazard (Piazon 60), Moses (Traore 46); Ba (Lukaku 46).
Mabao yametiwa kambani na: Hazard (penalty) 21, Ramires 29, 56 Ba 32, Terry 45, Traore 50, Lukaku 52, 65.
Bao la Indonesia All-Stars limefungwa na Kalas (og) katika dakika ya 67.
Raha tupu: Wallace, Demba Ba na Ramires wakishangilia bao
Haya si ndio mambo?: Nahodha John Terry akishangilia na Gary Cahill
Hapa hakuna uzalendo tena: Mashabiki nchini Indonesia wakishangilia wakati Chelsea akiwaadhibu All-Stars
Bosi: Jose Mourinho akitoa maelekezo kwa vijana wake
Wakali wa The Blues : Marco Van Ginkel, Gary Cahill na John Terry wakishangilia
Tabasamu kali: Jose Mourinho akiangalia vijana wake jinsi wanavyotoa kichapo mjini Jakarta
Nahodha: John Terry (kulia) akishangilia bao lake
Hakuna makosa: Eden Hazard alifunga bao la kwanza kwa njia ya mkwaju wa penati
Ramires akiandika kimiani bao
Mazoezi tu haya kijana: Demba Ba (kushoto) na Ramires wakishangia bao la tatu la Chelsea
0 comments:
Post a Comment