Na Baraka Mpenja kwa Msaada wa Sportsmail.com
MLINDA mlango mkongwe, Mark Schwarzer, ameihama rasmi klabu yake ya Fulham inayoshiriki ligi kuu soka nchini England baada ya mkataba wake kumalizika na kumwaga wino darajani katika klabu ya Jose Mourinho, Chelsea ya jijini London.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 40 aliwahi kuzichezea klabu za Bradford City, Middlesbrough pamoja na Fulham, na amecheza soka kwa mwaka wa 17 sasa huku akiwa na kiwango cha juu muda wote.
Schwarzer ameandika katika mtandao wa kiofisi wa klabu ya Chelsea kuwa klabu hiyo ni kubwa sana na moja kati ya timu bora zaidi duniani, hivyo kusaini mkataba na matajiri hao wa London ni heshima kubwa sana na hakutaka kupoteza nafasi hiyo.
Mlinda Mlango mkongwe: Mark Schwarzer amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea klabu ya Chelsea
Dili limekamilika: Schwarzer akisaini mkataba wake wakiwa na mkurugenzi wa timu David Barnard
Schwarzer ameweka wazi kuwa kurudi kwa kocha Mourinho kumemshawishi kujiunga na klabu hiyo bora katika taifa la England, hivyo ataitumikia kwa njia iliyotukuka.
Ameumabia mtandao wa Sky Sports: “Nimezungumza na kocha wa Chelsea na ilikuwa kazi nyepesi kufanya maamuzi kuikubali timu sahihi kwangu, uwezo na malengo ya klabu vimenishawishi zaid. Ni kama maajabu vile kusaini klabu bora”.
Kipa huyo raia wa Australia ameisadia timu yake ya taifa kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia mwakani 2014, na sasa atacheza sambamba na kipa namba moja wa Chelsea Petr Cech, lakini bado ataweza kupata nafasi ya kuonesha ubora wake.
Ameichezea mechi 108 timu yake ya Taifa, na akiwa England ameshinda kombe la Ligi akiwa na Middlesbrough mwaka 2003 , pia amecheza UEFA mwaka 2006 na ligi za Ulaya.
Wakitaniana: Schwarzer alikutana na wajembe ya England, Frank Lampard na John Terry
Anakutana na bosi: Jose Mourinho alifurahi kuonana na kifaa chake kipya
Watakaa langoni: Schwarzer akiwa na kipa mwenzake mpya Petr Cech
Karibu sana braza: Mshambuliajia raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku akimpa hai Schwarzer katika uwanja wao wa mazoezi wa Cobham
0 comments:
Post a Comment