Friday, July 26, 2013


Pix 1Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akisisitiza jambo wakati akizungumza na wabunifu (hawapo pichani) kutoka studio mbalimbali zinazojishughulisha na ubunifu wa utengenezaji wa matangazo na picha za juu ya kava za DVD na wawakilishi wa Steps na Pilipili Entertainment jana jijini Dar es Salaam.
Pix 3Mkurugenzi Mtendaji i-view studio Bw. Raqey Mohamed akiunga mkono suala la kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha kuwa wabunifu wa matangazo na picha za juu ya kava za DVD wanazingatia maadili jana jijini Dar es Salaam.
Pix 4Mkaguzi wa filamu kutoka Pilipili Entertainment Bi. Mwamvita Kituka akiwahasa wabunifu wenzake kulinda utamaduni wa mtanzania wakati wa kikao kilichowahusisha wakaguzi wa filamu kutoka bodi ya filamu na wabunifu wa matangazo na picha za juu ya kava za DVD jana jijini Dar es Salaam. 
Picha zote na Genofeva Matemu – MAELEZO
………
 
Na Genofeva Matemu – MAELEZO
WATAALAM wa kubuni matangazo na picha za filamu  juu ya kava za DVD na matangazo ya filamu wametakiwa kufuata Sheria ya Filamu  na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976  na kanuni zake ambayo inaitaka Bodi ya Filamu kutoruhusu kutumika picha za juu ya kava za filamu na matangazo zitaonyesha utupu ama kuonyesha maungo ya ndani ya wasanii. 
 
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo alipokutana na wabunifu hao ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumzia utengenezaji wa matangazo na kava zenye mwelekeo wa kudhalilisha, heshima na utu wa waigizaji, picha zenye kutoa taswira au hisia za ngono, picha zinazoonyesha uvaaji usio na staa unaodhalilisha heshima na utu wa mtanzania pamoja na picha zinazoonyesha maadili potofu na yasiyo katika maadili ya mtanzania.
 
Akijibu maswali tofautitofauti kutoka kwa wabunifu hao Bibi. Fissoo amewataka kuwa wabunifu huku wakiangalia kwa kina ubunifu huo hauvuki mipaka na kuharibu maadili ya mtanzania kwani bodi ya filamu haitaruhusu matangazo yenye picha za aina hiyo. Aidha Bodi isingependa kuzuia kazi za wadau wake kwani moja ya majukumu ni pamoja na kukagua na kutoa kibali kwa kazi za filamu na pia kuwawezesha wadau walioshiriki katika kazi husika kupata haki yao stahiki.
 
“Kukagua filamu na kutoa kibali haitoshelezi lengo letu lingine ni kuhakikisha kuwa tunawasaidia wadau walioshiriki kutoa filamu kupata jasho lao na kwa upande wa wafanyabiashara za uuzaji wa CD za filamu na picha jongevu kwa ujumla kupata haki stahiki” Amesema Bibi Fissoo. 
Kwa upande wake Mrakibu Msaidizi wa Polisi kutoka Polisi Makao Makuu Bw. Andrew Makungu amewataka wabunifu hao kuachana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea bali kuzingatia wajibu wao ipasavyo ili waweze kuondokana na makosa yanayojitokeza mara kwa mara na kuachana na kauli ya sikujua kwani kutokujua sher sio kinga.
 
Aidha Bw. Makungu amewahasa wabunifu hao kuwakumbusha wadau wengine kwenye tasnia ya filamu kupitia sheria ya filamu ya mwaka 1976 mara kwa mara ili kuepukana na matatizo yanayoweza kujitokeza baada ya filamu zao kupitiwa na bodi ya filamu kwa kupeleka kazi zao kukaguliwa na bodi kila wanapotoka hatua moja kwenda nyingine ili wawe ndani ya mstari wakati wote.
 
Naye mkaguzi wa filamu kutoka Pilipili Entertainment Bi. Mwamvita Kituka amesema kuwa kuweka picha za utupu haswa za wanawake katika kava za CD si utamaduni wa mtanzania bali ni kuwarithisha urithi mbovu watoto wetu na kuwasababishia kuwa na fikra potofu kimaadili.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video