Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mshambuliaji hatari wa Tottenham Gareth Bale amebaki mdomo wazi baaada ya klabu yake kukataa ofa ya pauni milioni 82 ambayo ingevunja rekondi ya uhamisho duniani kutoka kwa miamba ya soka la Hisapania na Ulaya, Real Madrid.
Bale mwenye miaka 24 aliikosia mechi ya kirafiki ya jana jumamosi mjiji Hong Kong na kujiona kama hatavaa tena uzi mweupe wa Tottenham .
Meneja wake Andre Villas Boas alikubaliana na nyota huyo raia wa Whales kutocheza michezo ya wiki hii ya Ubingwa wa Barclays Asia kwa madai ya kuwa majeruhi. Lakini ukweli ni kwamba Bale ni mzima wa afya, ila hayuko sawa kiakili kwani anawaza kuondoka.
Bale nje: Je, Bale ataonekana tena na uzi mweupe wa Tottenham?
Moyo wa Bale unawaka moto kwa kutaka kwenda Real Madridi ili ikacheze ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na nyota wa dunia Cristiano Ronaldo, Mesut Ozil, Luka Modric na Karim Benzema.
Lakini maamzi ya mwisho kutimiza ndoto yake yapo chini ya mwenyekiti wa Spur, Daniel Levy, ambaye ana roho ngumu ya kumuachia nyota huyo ambaye anataka amalizie miaka mitatu katika mkataba wake.
Bale ambaye atakosa fainali za kombe la dunia mwakani, sasa anataka kujipima uwezo katika michuano mikubwa ya UEFA, na anachukizwa na kitendo cha kushiriki mara moja tu mpaka anaelekea miaka 25.
Alikosa mechi : Bale alikosa mechi ya jana ambayo Spurs walishinda kwa mabao 6-0 dhidi ya South China
Bale, aliyeifungia mabao 31 klabu yake msimu uliopita, kwa sasa hataki kuongeza mkataba mpya na Spurs hata kama utakuwa na kopengele cha kuuzwa baadaye, kwani malengo yake ni kuihama.
Bale anataka kujiunga na Cristiano Ronaldo, Real Madrid
0 comments:
Post a Comment