Na Baraka Mpenja
Baada
ya kushuka daraja msimu uliopita, Klabu ya Africa Lyon ya jijini Dar es
salaam imeanza programu ya kutafuta wachezaji wapya kwa ajili ya msimu
ujao wa ligi daraja la kwanza.
Mmiliki wa klabu hiyo Rahim Rangezi Zamunda amezungumza na MATUKIO DUNIANI
na kusema kuwa malengo yao ni kuirejesha timu ligi kuu, hivyo wamewaita
wachezaji mbalimbali ili wajaribu bahati yao, na kwa yeyote atakayefaa
basi watamsajili.
“Sisi
tunajipanga vizuri, kila kitu kinaenda sawa, na leo hii tumefanya
mazoezi na vijana wapya, tutapata wazuri na kuwasajili kwa ajili ya ligi
daraja la kwanza”. Alisema Zamunda.
Zamunda
aliongeza kuwa kwa sasa wanahitaji kupata kocha mpya wa kigeni ili
aimarishe kikosi chao, lakini mipango yao iko pole pole kwani hawaitaji
haraka.
“Watu
wanachanganya, Charles Otieno hakuwa kocha wetu kwa muda ule, yeye ni
mkurugenzi wa ufundi wa klabu, kwa sasa yupo nchini Kenya kwa mapumziko,
tunahitaji kocha wa kufanya kazi nasisi, na Mkenya huyo atabaki kuwa
mkurugenzi wa ufundi”. Alisema Zamunda.
Mmiliki
huyo alisema wachezaji wote waliokuwepo klabuni hapo kwa Mkopo, ni
mmoja tu, Ibrahim Job ambaye ameombwa kubakia ili awape msaada.
Katika
hatua nyingine Zamunda alisema wachezaji wao wengi wataendelea
kuitumikia klabu katika kipindi hiki cha mapambano na uhakika wa maslahi
upo.
“Nimejiandaa
vizuri kuwalipa mishahara, posho na huduma nyingine za kibinadamu, pesa
ipo, cha msingi watambue kazi yao na wajitume zaidi”. Alisema Zamunda.
Katika
kikosi cha klabu hiyo Zamunda alisema wanahitaji zaidi wachezaji wa
safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa butu sana, halafu wanataka kusajili
walinzi wa ukweli ili kuweka mambo safi ligi daraja la kwanza msimu
ujao.
0 comments:
Post a Comment