Friday, June 7, 2013


003

Miza Othman na Mwanaisha Muhammed,  Maelezo-Zanzibar

ZAIDI ya shilingi milioni nne zinahitajika kwa ajili ya kulipatia ufumbuzi tatizo la kuharibika kwa mnara wa kurushia matangazo ya masafa ya kati katika redio ya Shirika la Utangazaji Zanzibar ulioko
Bungi Wilaya ya Kati Unguja.
Hayo yameelezwa na Fundi Mkuu wa ZBC Redio Ali Aboud Talib, mbele ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk, alipofanya ziara huko Bungi kuona uharibifu uliosababisha kukosekana
kwa matangazo hayo kwa mwezi mzima sasa.
Aboud amesema hali hiyo imetokana na kuharibika kwa kifaa cha kebo ya frikwensi, kinachotumika kusambazia matangazo  ya redio ya ZBC kwa
masafa ya kati.
Mapema, Waziri Mbarouk amelitaka Shirika la Utangazaji Zanzibar kufanya jitihada za haraka kulipatia ufumbuzi wa haraka tatizo hilo, ili kuwaondoshea usumbufu wananchi wa Zanzibar ambao hutegemea zaidi
redio hiyo.
Amesema lengo la serikali ni kuona wananchi wake wanapata matangazo ya redio yao ya taifa kwa siku na muda wote na kwa karibu zaidi.
Kwa hivyo, amewataka watendaji wa shirika hilo kujipanga na kuhakikisha tatizo hilo linarekebishwa kwa hali na mali na kama likishindikana nguvu za ziada zitatumika ili kurejesha matangazo ya
masafa ya kati.
Waziri huyo pia amesisitiza kuwepo ushirikiano kati ya wafanyakazi wa shirika hilo ili kunapotokea tatizo liweze kutatuliwa ipasavyo.
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR 7/6/2013

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video