Na Baraka Mpenja
Mabingwa
wa ligi kuu soka Tanzania bara na mabingwa watetezi wa kombe la Kagame,
Dar Young Africans wanaendelea vizuri na mazoezi yake ya kujiandaa na
michuano ya kombe la Kagame licha ya nyota wake muhimu kukosekana
kufuatia kuwa na majukumu ya timu za taifa.
Katibu mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameimbia MATUKIO DUNIANI Kuwa
klabu hiyo haiangalii Kagame tu bali wana mipango mingi hususani
ushiriki wao katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani.
Mwalusako
alisema wanajiandaa kushiriki michuano ya kimataifa, kutetea ubingwa
wao msimu ujao na kombe la Kagame mwaka huu, hivyo watu wanaosema Yanga
wanajiandaa na Kagame tu, wanatakiwa kukaa kimya.
“Yanga
tuna mipango mingi sana, Kagame sio kitu kwetu, lakini tunajipanga
sana, tunashiriki michuano mikubwa zaidi ya Kagame, tunatakiwa kufanya
vizuri zaidi michuano ya kimataifa ili kujenga heshima kwa mataifa
mbalimbali barani Afrika”. Alisema Mwalusako.
Katibu
huyo wa wanajangwani aliongeza kuwa kwa sasa wachezaji kadhaa wa kikosi
cha kwanza wapo na timu ya taifa ya Tanzania nchini Morocco, huku wale
wa kimataifa wakiwa na timu zao za taifa akiwemo Haruna Niyonzima,
lakini watakaporejea mambo yatazidi kunoga zaidi.
Pia
Mwalusako aliongeza kuwa baada ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu
uliopita, wanaandaa ziara ya mikoani kwa lengo la kuongea na wanachama
wao pamoja na kuwaonesha kombe lao.
“Tutapita
mikoa mbalimbali hapa nchini, lengo ni kuwaonesha ubingwa wetu na
kuongea nao kwa lengo la kujenga umoja na mshikamano wa klabu yetu,
tunaandaa ziara hiyo na mambo yanakwenda vizuri”. Alisema Mwalusako.
Yanga
wataiwakilisha Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani
Afrika msimu ujao baada ya kuwapokonya watani wao wa jadi ubingwa ,
wekundu wa Msimbazi Simba waliomaliza katika nafasi ya tatu kigumu sana,
baada ya kukabwa koo na Kagera Sugar kwa muda.
Michauno
ya mwaka huu Simba waliiwakilisha Tanzania na kutolewa hatua ya awali
baada ya kufungwa na Libolo ya Angola bao 1-0 uwanja wa taifa Dar es
salaam, na mechi ya marudiano walipigwa bao 4-0 nchini Angalo.
Mwaka ujao ni zamu ya Yanga kucheza ngoma hiyo nzito barani Afrika.
0 comments:
Post a Comment