Monday, June 3, 2013

IMG_9203 

Na Baraka Mpenja
Mabingwa wa kutandaza kandanda Tanzania Bara na Afrika Mashariki na Kati, Dar Young Africans wanatarajiwa kuanza mazoezi kwenye Uwanja wa shule ya sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam baada ya mapumziko mafupi kufuatia kumaliza msimu wa ligi kuu soka Tanzania bara mei 18 mwaka huu.
Katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako amesema wachezaji wote wanajua kuhusu kuanza kwa kambi hiyo ya kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame pamoja na msimu mpya wa ligi.
“Tuliwapa mapumziko ya wiki mbili na kila mchezaji anajua hilo, leo hii tunaanza kambi ya kujiwinda na Kagame, tunajua tuna kazi kubwa ya kutetea ubingwa wetu, lakini kila kitu kitaenda sawa”. Alisema Mwalusako.
Mwalusako alisema katika mazoezi ya leo watawakosa wachezaji wao wengi waliopo kikosi cha kwanza kwani wapo katika majukumu ya kuitumikia timu ya taifa.
Baadhi ya wachezaji hao ni  kipa Ally  Mustafa ‘Barthez’, mabeki Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, viungo Frank Domayo, Mrisho Ngasa, Simon Msuva na Athuman Iddi ‘Chuji’ walio Taifa Stars ya Tanzania.
Nyota wa kimataifa ni Haruna Niyonzima na Mbuyu Twite walio katika timu ya taifa ya Rwanda, wakati Hamisi Kiiza aliye na Uganda, amemaliza mkataba wake na mustakabali wake bado haujawekwa wazi katika klabu hiyo. 
Mwalusako alisema Kocha Mholanzi, Ernie Brandts anatarajiwa kuwasilia leo  baada ya mapumziko, lakini hata kama atakuwa hajafika, Kocha Msaidizi, Freddy Felix Minziro ataongoza mazoezi.
Katika hatua nyingine, Mwalusako alisema waliunga mkono tamko la waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Mhe. Bernad Membe kuhusu wasiwasi wa serikali ya Tanzania kuhusu hali ya usalama nchini Sudan hususani Darful.
“Kabla ya serikali kutoa tamko, tulikuwa tumeshaandika barua kuhusu wasiwasi wetu, mpaka waziri anasema tulikuwa hatujapata majibu, tunadhani Darful sio eneo salama, tunasubiri majibu ya mwisho”. Alisema Mwalusako.
Yanga ambao ni mabingwa mara mbili mfululizo wa Kagame, wamepangwa Kundi C katika michuano hiyo pamoja na Ports ya Djibouti, Express ya Uganda na Vital ‘O’ ya Burundi, wakati wapinzani wao wa jadi, Simba SC wamepangwa Kundi A pamoja na wenyeji El-Mereikh, Elman  ya Somalia na APR ya Rwanda
Katika michuano hiyo inayotarajiwa kuanza Juni 18 hadi Julai 2, mwaka huu mjini Khartoum, Sudan, mabingwa wa Kenya, Tusker wamepangwa Kundi B pamoja na wenyeji wengine, Al-Hilal, Falcons ya Zanzibar, Al Ahly Shandy ya Sudan na Al-Nasir Juba ya Sudan Kusini.
Mabingwa watetezi, Yanga wataanza kampeni zao za kutetea taji hilo Juni 20 kwa kumenyana na Express, wakati Simba SC itashuka dimbani Juni 21 kufungua dimba na El-Mereikh, na mechi zote zitachezwa Elfashar.

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video