Kaimu Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Neema Rusibamayila
(kushoto), akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, wakati akifungua mafunzo kwa wanahabari kuhusu umuhimu wa kutumia dawa za kinga, tiba ambazo zitaanza kutolewa bure juni 22 hadi 27 mwaka huu na wizara hiyo katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mwanza kupitia mpango wa taifa wa kutokomeza magonjwa ambayo yalikuwa hayajapewa kipaumbele (NTD’s). Kulia ni Mratibu wa Taifa wa magonjwa hayo, Dk. Upendo Mwingira

Mratibu wa Taifa wa magonjwa hayo, Dk. Upendo Mwingira,akitoa mada kwenye semina hiyo
Watoa mada katika semina hiyo kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiwa katika picha ya
pamoja na wanahabari waliohudhuria semina hiyo ya siku moja

(Na Philemon solomon wa Fullshangwe)
Wizara
ya afya na ustawi wa jamii kupitia Mpango wa taifa wa kudhibiti
magonjwa yaliyo kuwa yahapewi kipaumbele, imeendesha warsha ya siku moja
iliofanyika kwenye ukumbi wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa magonjwa ya
binadamu jijini Dar es salaam jana, kwa wahariri na waandishi wa vyombo
vya habari hapa nchini Kuhusu ugawaji wa dawa za matende na mabusha
katika mikoa ya Dar es salaam na mwanza.
Akifungua
warsha hiyo kaimu mkurugenzi kinga wa wizara hiyo Dr. Neema
Rusibamayila amesema kuwa, ugonjwa wa Matende, Ngiri, Minyoo ya tumbo,
Kichocho, Trakoma na usubi kwa muda mrefu yamekuwa hayapewi umuhimu
unaostahili kama magonjwa mengine na wadau wa afya hapa nchini, jambo
linalofanya yaendelee kusambaa katika mikoa mbalimbali na kuiathiri
jamii.
Aidha
Dr.Neema amesema kutokana na magonjwa hayo kuwa tishio kubwa katika
jamii, wizara hiyo mkupitia mpango wake wa kudhibiti magonjwa hayo
imeandaa mkakati wa kuyatokomeza hapa nchini ifikapo mwaka 2020.
Kwa
upande wake mratibu wa taifa wa mpango wa kudhibiti magonjwa
yaliyosahaulika Dr.Upendo Mwingira amsema endapo jamii itapata elimu na
kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali kupitia mpango huo, ni
dhahiri kwamba magonjwa yatakomezwa na kubakia kuwa historia.

0 comments:
Post a Comment