KLABU
ya Arsenal baada ya kumalizana kwa dau la Pauni Milioni 22 na Gonzalo
Higuain kutoka Real Madrid, sasa inahamishia nguvu zake kwa mshambuliaji
wa Manchester United, anayeuzwa Pauni Milioni 20, Wayne Rooney – huku
kocha Arsene Wenger akiwa amedhamiria kuendelea kumtumia katika nafasi
ya kiungo mshambuliaji nyuma ya Muargentina huyo.
Higuain
ni mchezaji ambaye Arsenal sasa wana uhakika wa kumnasa, huku Carlo
Ancelotti kocha mpya wa vigogo hao wa Hispania, akitarajiwa kutua leo
kuthibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo Bernabeu.
Matawi ya juu: Lakini mustakabali wa Wayne Rooney bado haueleweki
Lakini
katika uhamisho huo wa Rooney, Arsenal italazimika kumlipa mshahara
wake wa Pauni 220,000 kwa wiki, ambao ni mkubwa mno kulingana na
tamaduni za Arsenal, imekuwa klabu ‘bakhili’.
Wenger
haoni kama Rooney ni mshambuliaji wa kati, lakini kama kiunganishi,
baina ya kiungo na Higuain — nafasi ambayo mchezaji mwenyewe amesema
inamfaa.
Lakini
Chelsea pia inamtaka Rooney na kocha mpya wa United, David Moyes
anatarajiwa kukutana na Rooney wiki mbili zijazo, hivyo uwezekano wa
yeye kujiunga na klabu hiyo ya London bado mdogo.
United
haitataka kumuuza Rooney kwa Chelsea, ambao wanatarajiwa kuwa
washindani wao wakuu katika mbio za ubingwa na matumaini ya mchezaji
huyo yanabakia katika kikao chake na Moyes kwamba anaweza kupata mwanzo
mpya mzuri Old Trafford, hususan baada ya klabu kusema hajawahi kuomba
kuondoka United.
Hilo
ni suala lililotokana na wasiwasi wa Rooney juu ya uhusiano wake na
mashabiki wa United. Rooney anatarajia kikao kama alichowahi kufanya na
kocha aliyetangulia, Sir Alex Ferguson mwishoni mwa msimu uliopita, cha
binafasi kujadili mustakabali wake katika klabu.
Arsenal
imetenga bajeti ya kutosha kupambana katoka soko la usajili, lakini
tatizo ni kwamba wataweza kuwashawishi wachezaji wanaowataka, kwa sababu
ni wenye kiu ya mataji, vitu ambavyo kwa sasa klabu hiyo vimekuwa
adimu.
Mzee wa matarajio: Arsene Wenger wa Arsenal yuko tayari kugombea saini ya Rooney.
0 comments:
Post a Comment