Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt Fenella Mukangara (kulia)
akimkabidhi Katibu wa Jumuiya ya Wanawake CCM (UWT) Kata ya Ubungo Bi
Rose Ndunguru (Kushoto) Jumla ya Jezi seti mbili na Mipira tisa
ilikabidhiwa ikiwa ni msaada kwa ajili ya Mashindano mpira wa Pete ya
Kombe la Mheshimiwa Riose Wassira iliyoanza kuanzia jana katika viwanja
vya Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt Fenella Mukangara (kulia)
akimkabidhi Katibu wa Jumuiya Wanawake CCM (UWT) Kata ya Ubungo Bi
Rose Ndunguru (Kushoto) Jumla ya Jezi seti mbili na Mipira tisa
ilikabidhiwa ikiwa ni msaada kwa ajili ya Mashindano mpira wa Pete ya
Kombe la Mheshimiwa Riose Wassira iliyoanza kuanzia jana katika viwanja
vya Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Mhe.Dkt Fenella Mukangara (kulia)
akimkabidhi Katibu wa Jumuiya Wanawake CCM (UWT) Kata ya Ubungo Bi
Rose Ndunguru (Kushoto) Jezi kwa ajili ya Mashindano ya mpira wa Pete
yanayojulikana kwa jina la Kombe la Mheshimiwa Rosea Wassira
yanayofanyika katika viwanja vilivyopo Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam
PICHA ZOTE NA FRANK SHIJA – MAELEZO
Na Frank Shija – Maelezo
Serikali
itaendelea na juhudi zake za kuhakikisha inakuza sekta ya michezo nchini
kwa kuhakikisha inasaidia ukuaji wa michezo mbalimbali na kuhamasisha
vijana kujihusisha na shughuli za michezo ambayo inaonekana kutotiliwa
mkazo.
Kauli hiyo
imetolewa na Waziri wa Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt Fenella
Mukangara alipokuwa akikabidhi vifaa vya michezo kwa ajili ya mashindano
ya mpira wa Pete yanayojulikana kama Mheshimiwa Rose Wassira Cup jana
jijini Dar es Salaam.
Waziri Fenella
amesema kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kuhakikisha sekta ya michezo
inakua nchini na kupitia Wizara yake Serikali imekuwa ikitoa misaada
pale panapohitajika.
Aidha Mheshiwa
Fenella ameongeza kuwa kuna dhana potofu imejengeka miongoni mwa jamii
kuwa Serikali imekuwa ikitoa kipaumbele kwa mchezo wa Soka pekee na
kusema kuwa Serikali imekuwa ikijitahidi kusaidia michezo mbalimbali na
kuvitaka vyama vya michezo husika kujidhatiti badala ya kujiweka kando
na kuitupia lawama Serikali.
“Naomba niweke
sawa suala moja muhimu hapa,kumekuwa na kasumba ya watu kusema kuwa
Serikali inapembelea mchezo wa Soka pekee na kusahau mingine, suala hili
siyo sahihi kwani kupitia Wizara yangu Serikali imekuwa ikishirikiana
na wadau na viongozi mbalimbali wa vyama vya michezo kuhakikisha sekta
hii inakua, mtakumbuka majuzi tu nilishiriki kuwaaga wachezaji wa mchezo
wa Gofu walioenda kwenye mashindano ya kimataifa sasa hapo mnasema
tunapendelea Sokapekee” . Alisema Waziri Fenella.
Kwa upande
wake Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Kata ya Ubungo Bi Rose
Ndunguru amemshukuru Waziri Fenella kwa msaada wake wa vifaa hivyo na
kusema kuwa vitaongeza hamasa katika mashindano hayo.
Katibu huyo
ameongeza kuwa kwa msaada wa vifaa hivyo imejidhihirisha wazi kuwa
sikweli kwamba serikali inapendelea aina Fulani ya mchezo kwani msaada
huo umetolewa kwa ajili ya mchezo wa mpira wa Pete ambao ni miongoni mwa
michezo inayoonekana kama imesahaulika.
Rose ameongeza
kuwa imefika wakati wadau na wapenda maendeleo ya michezo kushirikiana
badala ya kutupa lawama kwa serikali kwani kufanya hivyo siyo kuitendea
haki kwakuwa ni ukweli usiopingika kuwa imekuwa ikijitahidi kuhakikisha
michezo inakua hapa nchini.
Jumla ya seti
mbili za Jezi na mipira tisa ilikabidhiwa kwa ajili ya mashindano ya
Kombe la Mheshimiwa Rose Wassira yaliyoanza jana katika viwanja vya
Ubungo Msewe jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment