Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Wakati
klabu za Manchester United, Chelsea na Real Madrid zikihaha kumsaka
mshambuliaji nyota wa Borrusia Dortmund, Roberto Lewandowski ili
kumsajili msimu ujao wa ligi, leo hii meneja mkuu wa klabu hiyo
Hans-Joachim Watzke amesema nyota huyo atakataa kujiunga na United
majira ya joto ya usajili ya mwaka huu.
Nyota
huyo tayari ameshaonesha nia ya kujiunga na mabingwa wa Bundesliga na
ligi ya mabingwa barani ulaya, Bayern Munich msimu ujao, ingawa Watzke
hajamuambia chochote kuhusiana na nia yake ya kuhamia kwa wekundu hao wa
Allianz Arena.
Nyota huyo aliyejizolea sifa kubwa mwaka huu katika michauno ya UEFA baada ya kuwafunga Real Madrdi
Watzke
amesema klabu zinazomuwania nyota huyo kwasasa zinapoteza muda na
zinatakiwa kuangalia mambo mengine kwani kwa sasa Robert hawezi kuihama
klabu yake.
“Robert ataichezea klabu yake ya Borussia Dortmund msimu ujao”. Watzke ameliambia gazeti za Ujerumani la Suddeutsche Zeitung.
Hatoki mtu hapa! Robert Lewandowski anataka kubakia Borussia Dortmund msimu ujao
0 comments:
Post a Comment