Wajumbe
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) jana walifanya ziara
katika ofisi za Makao Makuu ya Mfuko huo kwa lengo la kutembelea ofisi
hizo na kuangalia mazingira ya kazi.
Wajumbe
walioteuliwa hivi karibuni wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo,
Balozi Ali Mchumo, Mwanaidi Mtanda, Ezekiah Oluoch, Donan Mmbando,
Mohamed Mohamed, Lydia Choma, Mohamed Hashim, Charles Kajege na Emanuel
Humba ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo.
Wajumbe
wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wakipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti Raphael Mwamoto walipozuru
Makao Makuu jana. Mwenyekiti
wa Bodi, Balozi Ali Mchumo (wa tatu kutoka kulia) akipata maelezo ya
uwekezaji uliofanywa na NHIF kutoka kwa Mkurugenzi wa Fedha na Uwekezaji
Bw. Rutazaa.
Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Emanuel Humba akiongozana na Mwenyekiti wa Bodi Balozi Mchumo kukagua maeneo ya Mfuko huo Mkurugenzi
wa Uendeshaji, Eugen Mikongoti akitoa maelezo ya namna ya kuhifadhi
kumbukumbu za wanachama katika kituo cha kisasa cha Mfuko huo.
Wajumbe
hao wakipata maelezo kutoka kwa Ofisa wa NHIF namna ya upatikanaji wa
haraka wa kumbukumbu za wanachama zinazohifadhiwa katika kituo hicho.
Wajumbe wakiendelea kujifunza zaidi katika kituo cha kuhifadhia kumbukumbu. Mkurugenzi Mkuu Emanuel Humba akifafanua jambo wakati wa ziara hiyo.
0 comments:
Post a Comment