Ujumbe
wa wabunge watano kutoka Uingereza umewasili nchini na kutembelea Chuo
Kikuu cha Dodoma kujionea mandeleo yake. Baada ya kupokelewa uwanja wa
ndege wa Dodoma na Mwenyekiti wa CPA tawi la Tanzania Mhe. Mussa Azzan
Zungu, wabunge hao wakiwa na wenyeji wao walikutana na Makamu Mkuu wa
UDOM Prof. Kikula na baadaye kufanya ziara fupi kwenye hospitali ya Chuo
kitengo cha matibabu ya figo na sehemu ya utakasaji wa maji
yanayotumika kwa upasuaji. Ziara ya UDOM iliitimishwa dhifa fupi
iliyoandaliwa na Ofisi ya Bunge ikiongowa na Naibu Spika wa Bunge Mhe.
Job Ngugai pamoja na Katibu wa TWPG na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria
Mhe. Angela Kairuki katika Hoteli ya Dodoma.
Na Prosper Minja – Bunge
0 comments:
Post a Comment