Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mabingwa
wa soka nchini Italia, Juventus, vibibi vya Turini wamemumweka katika
darubini yao mshambuliaji nyota wa klabu ya Manchester City ya England
raia wa Argentina Carlos Tevez endapo watashindwa kumpata nyota wa
Fiorentina ambaye pia anawaniwa na klabu za Arsena na Chelsea, Stevan
Jovetic.
Tevez
amebakiza mwaka mmoja tu katika mkataba wake, sawa na Javi Garcia, Edin
Dzeko na Joleon Lescott ambao kwa sasa wanasikilizia ofa za kusajiliwa.
Nyoya
Jovetic mwenye umri wa miaka 23 ana thamani ya kitita cha pauni milioni
30 na Juventus wana wasiwasi mkubwa wa kupigwa bao na matajiri wa
London wenye jeuri kubwa ya pesa, klabu ya Chelsea.
Si mchezo kabisa: Carlos Tevez anafukuziwa na vibibi vya Turin, Juventus ya Italia
Tevez
(kulia) akiwa na Joe Hart (kushoto), Vincent Kompany (katikati) na
Matija Nastasic (katikati kulia) wakiwa katika hafla maalumu ya klabu
yao
Anawazisha watu balaa: Stevan Jovetic ataamua wapi aende, Arsenal, Chelsea au Juventus
0 comments:
Post a Comment