Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Hatimaye
biashara kwisha kabisa, jijini London habari ya huko ni kurejea kwa
kocha, the spesho one, Jose Mourinho ambaye leo amesaini mkataba wa
miaka minne kuinoa klabu yake ya zamani ya Chelsea.
Kocha
huyo wa zamani wa klabu ya Benfica, FC Porto, Inter Millan na Real
Madrid amerejea katika klabu yake ya zamani aliyoochana nayo mwaka 2006
baada ya kutofautiana na bosi wake Roman Abramovich.
Baada
ya kumwaga wino katika karatasi ya mkataba wa miaka minne, Mourinho
amekiri wazi kuwa Chelsea ni klabu anayoipenda zaidi ikifuatiwa na Inter
Millan, na sasa anarejea kwa mara ya pili.
Mourinho
amesaini mkataba ikiwa ni masaa machache amalize kibarua chake santiago
Bernabeu, na leo hii amefurahi sana kurejea EPL.
Karudi mjini: Jose Mourinho akiwa ameshika jezi yake ya Chelsea akiwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea
Karibu nyumbani: Mourinho amekiri kuwa anaipenda zaidi Chelsea kuliko karibu zote duniani, ya pili ni Inter
Amerudi England: Jose Mourinho amemwaga wino kuifundisha Chelsea kwa miaka minne
Mechi ya mwisho: Jose Mourinho aliwapungia mkono wa bai bai mashabiki wa Real Madrid
0 comments:
Post a Comment