MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Carlos
Tevez anajiandaa kuhamia Juventus baada ya klabu hizo mbili kukubaliana
kuuziana mchezaji huyo kwa ada ya Pauni Milioni 10.
Viongozi wa mabingwa hao wa Serie A walisafiri hadi Uingereza usiku wa jana kukamilisha dili la kumchukua Muargentina huyo.
Tevez alikaribia kuondoka vibayakipindi cha nyuma City na sasa inatokea ataondoka vizuri Etihad baada ya makubaliano ya kumuuza.
Njiani: Carlos Tevez anajiandaa kuondoka England baada ya miaka saba akihamia Juventus
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 amebakiza mwaka mmoja Etihad na anaweza kuondoka bure katika klabu hiyo msimu ujao.
Tevez anatarajiwa kwenda Turin kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili huo.
Uhakika: Tevez amekuwa miongoni mwa wachezaji tegemeo wa Manchester City tangu alipowasili mwaka 2009
0 comments:
Post a Comment