Baadhi
ya watalii wakiwa katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujioea wanyama
mbalimbali ikiwemo makundi ya nyumbu wakati yakivuka mto Mara kurejea
katika hifadhi hiyo kutoka Maasai Mara.
Na Geofrey Tengeneza
Nyota
ya Tanzania katika sekta ya Utalii imeendelea kung’ara zaidi badaa ya
hivi karibuni kuchaguliwa kuwa ndio nchi bora kwa watu mbalimbali kuweza
kufanya safari za kitalii miongoni mwa nchi barani Afrika.
Kwa
mujibu utafiti uliofanywa na kutolewa hivi karibuni na katika mtandao wa
Kampuni ya marketplace kwa ajili ya safari za Africa (marketplace for
African safari tour)
Tanzania
imepata kura nyingi zaidi ziliyotolewa kama maoni ya watu kufuatia
utafiti huo ambapo Safaribooking .com ilifanya mchanganuo huo kwa
kupitia maoni 3061ya zaidi ya watalii na wasafiri waliohusishwa katika
utafiti huo na kuhitimisha kuwa katika nchi zote zilizopendekezwaa
barani Africa,Tanzania ni zaidi. Tanzania imekuwa ya kwanza kwa kupata
wastani wa alama 4.8 kwa nchi tano mashuhuri barani Africa kati ya nchi
nane zilizoshiriki. Botswana na Kenya zilipata wastani wa alama 4.7 kila
moja zikifuatwa na Africa kusini na Zambia zilizopata wastani wa alama
4.6 kila moja dhidi ya Namibia iliyopata wastani wa 4.5 na Uganda
kupata wastani wa 4.2 dhidi ya Zimbabwe iliyopata 4.2
Kama nchi bora kwa safari za kitalii baran Africa, Tanzania ikitazamwa pia kama lango bora
Miongoni
mwa sababu kubwa zinazotajwa kuchangia ushindi wa Tanzania ni pamoja na
baadhi ya vivutio vyake yake maarufu kama Hifadhi ya Taifa Serengeti na
Kreta ya ngorongoro ambavyo vimekuwa vikivutia watalii wengi kuja
kutoka sehemu mbalimbali Duniani. Serengeti ni makazi ya uhamiaji
mkubwa ambapo wanyama kama pundamilia na nyumbu huhama, alisema
Wouter Vergeer mmiliki wa tovuti huko nchin Netherland.
“Anaongeza
kuwa wasafiri na wageni wameipigia kura Tanzania kwa kuwa na sokwe
wengi Afrika na kwa kupokea wageni ambao huja kupanda mlima mrefu kuliko
yote Afrika mlima Kilimnajaro, na pia wageni hufurahia uhalisia wa
wanyama mwitu . Kuna uchaguzi huru wa safari kwa bajet yoyote na
mapumziko ya furaha katika kisiwa cha Zanzibar. Safari ni rahisi kwa
ndege katika kukamilisha mzunguko huo. Tanzania pia ni nchi iliyo imara
kisiasa na kiusalama”
Akiongea na Safaribooking
alisema anashangaa kuona kuwa watalii wanaweza kuitembeleaTanzania
kipindi chochote cha mwaka ikiwemo kipindi cha masika jambo ambalo
amesema limeifanya Tanzania kusifiwa na watalii wengi wanaotembelea
nchini. Mwandishi wa Six Lonely Planet guides to Africa Bi Mary
Fitzpatrick kutoka Marekani, aliwahi kuandika kuwa pamoja na wanyamapori
wake na vivutio vingine vizuri Tanzania imejaaliwa kuwa na viumbe
wazuri wa kila aina, miti aina ya acacia, mibuyu na mingine mingi
ambavyo vyote vinapamba sura ya nchi, na kuifanyaTanzania ni nchi bora
kwa safari Africa.
Hii
ni mara ya pili kwa Tanzania kung’ara barani katika sekta ya utalii
kwani itakumbukwa kuwa mwezi Februari mwaka huu Tanzania iliweka rekodi
ya aina yake pale vivutio vyake vyote vitatu vya Tanzania vilivyoingia
katika shindano la kutafuta Maajabu Saba ya Asili Barai Afrika ambavyo
ni Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (kwa maana ya nyumbu wahamao), Mlima
Kilimnjaro na Kreta ya Ngorongoro vilishinda na kuwa miongoni mwa
maajabu Saba ya Asili ya Afrika huku Hifadhi ya Taifa ya Serengeti
ikiongoza kwa kupigiwa kura nyingi zaidi.
0 comments:
Post a Comment