Taifa
Stars inatupa karata yake ya pili ugenini kwenye mechi za mchujo za
Kombe la Dunia kwa kesho (Juni 8 mwaka huu) kuikabili Morocco (Lions of
the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand Stade hapa Marrakech, Morocco.
Ilipoteza
ya kwanza ugenini dhidi ya Ivory Coast mwaka jana, na kushinda mbili
mfululizo nyumbani dhidi ya Gambia na Morocco. Mechi hiyo itakayochezwa
kuanzia saa 3 usiku kwa saa za Morocco ni ya pili kwa Stars katika
uwanja huo ambapo mwaka juzi ilifungwa mabao 3-1.
Washabiki
wa Morocco wanaonekana kuikatia tama timu yao yenye pointi mbili tu
nyuma ya Ivory Coast inayoongoza kundi hilo la C ikiwa na pointi saba
ikifuatiwa na Tanzania yenye sita. Huo ni mtazamo wa washabiki, lakini
kwa upande wa timu inaonekana imepania kujichomoa katika nafasi za
chini.
Kwa
upande wa Kocha wa Stars, Kim Poulsen amesema timu yake imepania mechi
hiyo, lengo likiwa ni kuona inapata matokeo mazuri baada ya dakika 90 za
mechi hiyo itakayokuwa chini ya refa Daniel Frazier Bennett wa Afrika
Kusini.
Amesema
timu yake itacheza kwa umakini na uangalifu kwa vile wanajua wapinzani
wao wakicheza mbele ya washabiki wao watakuwa katika shinikizo za
kushinda, jambo ambalo wamejiandaa kukabiliana nalo.
Kwa
upande wa maandalizi, Kim amesema Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) na wadhamini wa timu hiyo Kilimanjaro Premium Lager wameiandaa
vizuri kwani iko kambini kwa wiki tatu sasa na kupata mechi ya kirafiki
dhidi ya Sudan iliyochezwa wiki iliyopita nchini Ethiopia.
Stars
iliifunga Morocco mabao 3-1 zilipokutana Machi 24 mwaka huu jijini Dar
es Salaa. Lakini zilipokutana hapa Marrakech mara ya mwisho mwaka 2011,
Morocco iliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Kim
amesisitiza kuwa kikosi chake kimepania kufanya vizuri katika michuano
hii ya mchujo ya Kombe la Dunia, ha hiyo inathibitishwa na matokeo ya
timu kadri inavyoendelea kucheza mechi za mashindano.
“Moja
ya mipango yetu katika mechi hizi za Kombe la Dunia ni kushinda
nyumbani, hilo hadi sasa tumelifanya kwa asilimia 100. Lakini ili tukae
vizuri zaidi tumekuja hapa Morocco kwa lengo la kupata matokeo mazuri,
ingawa tunajua mechi itakuwa ngumi,” amesema kocha huyo raia wa Denmark.
Kwa
hapa Marrakech mechi hiyo imekuwa haizungumzwi mara kwa mara, na kubwa
ni kuwa Wamorocco wengi wanaamini kuwa timu yao ambayo hadi sasa ina
pointi mbili haina nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata ya
michuano hiyo.
0 comments:
Post a Comment