UWEZEKANO
wa mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Felix Sunzu kuendelea kuichezea
Simba ni finyu baada ya benchi la ufundi kusema halimuhitaji.
Sunzu
aliyetua Msimbazi Julai 2011, akitokea El Hilal ya Sudan baada ya
kung’ara kwenye michuano ya Chalenji, hatima yake imekuwa ikitiliwa
shaka kutokana na kiwango chake licha ya kulipwa mamilioni ya fedha.
Hata
hivyo, uongozi uliendelea kumvumilia nyota huyo wakihofia gharama za
kukatisha mkataba wake, hadi ulipomalizika baada ya kwisha kwa ligi Kuu
Tanzania bara, Mei 18.
Habari
kutoka ndani ya Simba zinaeleza kwa sasa nyota huyo hayupo kwenye
mipango ya klabu hiyo kwa msimu ujao, lakini anaweza kuongezewa mkataba
kama mipango ya kumsajili Mganda Moses Oloya itashindikana.
Chanzo
cha uhakika kutoka ndani ya Simba kimedokeza uwezekano wa Sunzu
kuongezewa mkataba upo mikononi mwa benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu
Abdallah ‘King’ Kibadeni na msaidizi wake Jamhuri Kihwelo ‘Julio’.
“Ni
kweli Sunzu amemaliza mkataba wake, lakini jukumu la kuendelea kuichezea
Simba au kuachana naye lipo mikononi mwa makocha, hivyo waulizwe wao
kwanza,” kilisema chanzo hicho.
Alipoulizwa
Julio kuhusu nyota huyo, alisema kwa aina ya wachezaji waliopo kwenye
kikosi chao, Sunzu hana nafasi kwa sababu namba anayocheza tayari ina
wazuri zaidi yake.
Julio
aliyewahi kuichezea Simba na Taifa Stars, alisema kwa sasa kikosi chao
kimekamilika kila idara, ndiyo maana Sunzu hana nafasi kwani imeshazibwa
na wengine.
Mbali
ya Julio, hata Kibadeni mara kadhaa amekuwa akisema hatamsajili
mchezaji wa kigeni hadi awe na uwezo wa ziada dimbani ambao nyota
wazalendo hawana.
Sunzu
aliyezaliwa Februari 5, 1989 katika kitongoji cha Chingola, Zambia
kabla ya kutua Simba alichezea timu za Konkola Blades, Marsa,
Châteauroux na El Hilal, pia ameichezea timu ya taifa ya Zambia mara 14
na kuifungia mabao nane.
CHANZO TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment