Sunday, June 16, 2013


0056
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Dakika tisini za mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil baina ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars dhidi ya Ivory Coast zimemalizika kwa Tembeo wa Afrika kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.
Mchezo huo umepigwa katika dimba maridadi la taifa jijini Dar es salaam na kushuhudiwa na maelfu ya mashabiki wa soka nchini Tanzania.
Licha ya kupoteza mchezo huo Stars imecheza vizuri na kuwasakama vilivyo wanaume hao kutoka pwani ya magharibi mwa Afrika.
Makosa ya uzembe ya safu ya ulinzi ya Stars iliyoongozwa na mabeki, Shomary Kapombe upande wa kushoto, Erasto Nyoni upande wa kulia na katikati wakisimama Kelvin Yondan na Nadir Haroub “Canavaro” yameigharimu Stars na kufunga mabao mepesi kabisa.
Mchezaji wa Manchester City inayocheza ligi kuu soka nchini England, Yaya Toure amefunga mabao mawili peke yake na kuleta kilio kwa watanzania wengi waliofurika uwanjani.
Kwa ushindi huo, Ivory Coast imetimiza pointi 13 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine yoyote katika kundi hilo na sasa itasubiri kucheza na mmoja wa washindi wengine wa makundi mengine tisa ili kuwania kwenda Brazil mwakani.
Tanzania inabaki na pointi zake sita, huu ukiwa mchezo wa kwanza kufungwa nyumbani katika kampeni hizi na Morocco bila kuhusisha matokeo yake na Gambo, ina pointi tano.  
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Mehdi Abid aliyesaidiwa na Hamza Hammou, Bauabdallah Omar wote kutoka Algeria, hadi mapumziko Ivory Coast tayari walikuwa mbele kwa mabao 3-2.
Stars ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao mfungaji Amri  Kiemba dakika ya kwanza tu aliyepokea pasi ya Mbwana Ally Samatta kufuatia mpira wa kurushwa na Erasto Edward Nyoni kusababisha kizazaa langoni mwa Tembo wa Abidjan.
Nyoni alirusha kama amepiga kwa mguu karibu kabisa na kibendera cha kona kufuatia beki Suleiman Bamba kumpitia Thomas Ulimwengu na kutoa nje na mpira ukaokolewa kabla ya kumkuta Samatta aliyempelekea mfungaji.
Ivory Coast wakasawazisha bao hilo dakika ya 15 kupitia kwa Lacina Traore baada ya mabeki wa Stars kuzembea kuokoa na Yaya Toure akafunga la pili kwa mpira wa adhabu dakika ya 23, nje kidogo ya eneo la hatari.
Bao hilo lilitokana na wachezaji wa Stars kupanga ukuta wao vibaya na kumpoteza maboya kipa wao, Juma Kaseja.
Stars ilirudi mchezoni na kufanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 35 mfungaji Ulimwengu aliyeunganisha krosi maridadi ya Shomary Kapombe.
Hata hivyo, Ivory Coast wakapata penalti rahisi baada ya Gervinho kujiangusha wakati anakabiliana na Nadir Haroub ‘Cannavaro’ Yaya Toure akaenda kumtungua Kaseja dakika ya 43.
Kipindi cha pili Stars ilikianza vizuri na kushambulia mara nyingi langoni mwa Ivory Coast, lakini wakaishia kukosa mabao ya wazi.
Mabadiliko yaliyofanywa na kocha Mdenmark, Kim Poulsen dakika ya 87 kumtoa kiungo Mwinyi Kazimoto na kumuingiza mshambuliaji Vincent Barnabas yaliigharimu Tanzania kwa kufungwa bao la nne na kupotea kabisa mchezoni.
Baada ya kutoka Kazimoto, aliyetekeleza majukumu yake vizuri leo, Ivory Coast wakatawala sehemu ya kiungo na kutengeneza bao la nne lililofungwa na Bonny Wilfred dakika ya 88.
Pamoja na kufungwa, Stars ilicheza soka safi ya kuvutia na mabao yote yalitokana na makosa – na si kuzidiwa uwezo. 
Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomary Kapombe/Khamis Mcha dk 85, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Frank Domayo, Mwinyi Kazimoto/Vincent Barnabas dk 87, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu, Mbwana Samatta na Amri Kiemba.
Ivory Coast; Boubakar Barry, Arthur Boca, Didier Zakora, Solomon Kalou/Sio Giovanni, Gervais Yao, Jean Jarques Gosso Gosso, Alain Aurier, Lacina Traore/Bonny Wilfred, Yaya Toure, Geoffrey Serey na Suleiman Bamba/Nori Koffi Christian. 

0 comments:

 
voyeur porn porn movies sex videos hd porno video