Washindi
wa Redds Miss Kinondoni Talent 2013 wakiwa katika sura za furaha mara
baada ya kuwagalagaza wenzao na kujikuta wanapatikana wao Kutoka Kulia
ni Sophia Yusuf, Phillious Lemi na Linda Joseph.
Jaji mkuu wa shindano hilo mtayarishaji wa Muziki, Man Walter akiwa na msaidizi wake wakati wa shindano hilo.
Na Cathbert Angelo, Kajunason Blog.
Jumla
ya washiriki watatu wamepatikana katika shindano Redd’s Miss Kinondoni
Talent 2013 lililofanyika katika ukumbi wa Shekinah Garden, Mbezi Beach
jijini Dar es Salaam.
Akitangaza
washindi hao, jaji mkuu wa shindano hilo mtayarishaji wa Muziki, Man
Walter aliwataja Sophia Yusuf, Phillious Lemi na Linda Joseph kuwa ndiyo
waliowagalagaza wenzao wapatao 10 waliokuwa katika kinyang’anyiro
hicho.
Nae
Muandaaji wa shindano hilo, Dennis Ssebo alisema kuwa fainali za
mashindano hayo zinafanyika leo Juni 21 mwaka huu katika uwanja wa
hoteli ya Golden Tulip.
Alisema
kwamba shindano la mwaka huu litaandika historia mpya ya urembo kwa
wilaya ya Kinondoni maana wamejipanga na kupata sapoti ya kutosha, hivyo
mashabiki wa mashindano ya urembo wakae mkao wa kupata raha.
Mashindano
ya Redd’s Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy
Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Kiota cha Maraha
WANTASH, Virago, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group,
Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog,
Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog,
Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.
Mambo ya maunooooo….
Aha! kila mmoja alionyesha umahili wake wa kuonyesha vituko, hapa ni nani kamwaga pombe yangu???
Bongiliiii bingiliiii mpaka chiniiiiiiiii….
…Mrithi wa Wanne sTAR akionyesha namna ya kula moto…
Segereeeee limenoga.
Muandaaji wa shindano la Redds Miss Kinondoni 2013, Dennis Ssebo akitoa machachee.
… huyu anafuata nyayo za Mrisho Mpoto
… kwenye Moja na Mbili ni Mwanadada Jenifa Kakolaki akimsaidiana na Dj
Wageni waalikwa…
…Kiuni bila mfupa
Matroni wa warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 akishangiliwa mara baada ya kuonyesha umahili wak e wa kucheza.
0 comments:
Post a Comment