Shomary
Kapombe (juu pichani) na Edward Christopher (Chini pichani) ni zao la
Morogoro Youth Soccer Academy, kwa vipaji vyao hawatakiwi kuishia Simba
Moja
kati ya walinzi bora wa pembeni wa klabu ya Yanga kwa sasa ni bwana
mdogo Juma Abdul(kushoto) ambaye ametokea kituo cha Morogoro
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Klabu
kongwe za kandanda nchini Tanzania, wekundu wa msimbazi, Simba na Dar
Young Africans “ Kwalalumpa Malysia” zimeshauriwa kuachana na kasumba ya
kuwabania wachezaji wao kwenda kucheza soka la kimataifa kwani kama nao
wangefanyiwa hivyo wasingesajili kwa mbwembwe kubwa.
Akizungumza na mtandao wa kazi wa FULLSHANGWE
mkurugenzi mkuu wa kituo cha kulea na kukuza vipaji kwa vijana wadogo
cha mkoani Morogoro, (Morogoro Youth Soccer Academy), Rajab Kindagule
amesema kuwa vituo vya soka kama kilivyo chake hujitahidi kuzalisha
wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, lakini wanapoenda katika klabu
za ligi kuu hususani Simba na Yanga wanaharibikiwa maisha yao ya soka na
kubaniwa kwenda kucheza nje ya nchi.
Kindagule
amesisitiza kuwa kituo chake ni kitalu cha kuzalisha wachezaji huku
akiwataja baadhi ya wachezaji wanaofanya vizuri kama Kiraka Shomary Kapombe na Edward Cristopher wanaocheza Simba, pia beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul kuwa ni zao la kituo hicho pamoja na wengine wengi wanaocheza ligi ligi kuu na daraja la kwanza.
“Kapombe
ni zao langu, nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa kijana anatakiwa
kwenda Uholanzi kufanya majaribio, chonde chonde Simba wasifanye mchezo
na kumbania bwana mdogo, wamuache aende kucheza huko na anaweza kupata
nafasi ya kwenda ligi kubwa zaidi”. Alisema Kindagule.
Mkurugenzo
huyo alisema iwe mwiko kwa wachezaji wanaotoka vituoni kuishia Simba na
Yanga, bali wanatakiwa kuendelezwa zaidi mpaka medani ya kimataifa ili
timu ya taifa ipate wachezaji mahiri zaidi mfano wa Samata na Ulimwengu.
“Sisi
tumeshakubaliana na wakala anayetaka kumpeleka Kapombe Uholanzi kuwa
anataka kujenga ushirikiano na kituo changu, ni nafasi nzuri sana kwa
wachezaji kwa sababu watakuwa wanapelekwa nchini humo kwa majaribio,
lakini lazima timu zetu zibadilike jamani”.
Kindagule
alisema kituo chake kinachukua vijana wadogo wa umri chini ya miaka 12
kitu ambacho kinawatofautisha na vituo vingine, hivyo juhudi kubwa
wanazotumia kuwaendeleza vijana zinapaswa kuendelezwa na timu
zinazowachukua vijana hao.
Pia
mdau huyo na kiongozi wa soka la vijana amekiri kuwa mipira waliyopewa
na rais wa shirikisho la soka Tanzania, injinia Leodigar Chilla Tenga
amewasaidia sana kuendeleza kituo na sasa mambo yanakwenda vizuri.
“Kama TFF wana uwezo, kila mwaka watusaidie kama alivyofanya Tenga, itatusaidia kufika mbali zaidi”. Alisema Kindagule.
Kindagule
aliongeza kuwa kwa sasa amesikia Rais wa Jamhuri ya Muungano
waTanzania, DKT.Jakaya Kikwete ana mpango wa kuanzisha Academy ya soka
nchini, lakini ametoa wito kwa Rais kutafuta watu makini kama akina
Kanali Idd Kipingu wenye dhati ya kuendeleza soka kuliko kuwapa wahuni.
“Tunahitaji
watu wenye nia ya dhati na moyo, wazalendo ili tuweze kufika mbali,
kama kutakuwa na wachumia matumbo, haina maana sasa”. Alisema Kindagule.
0 comments:
Post a Comment