Kijikio |
Maafande
wa Ruvu Shooting chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa “Masta”
wamendelea kutangaza vita kwa klabu za ligi kuu Tanzania bara msimu
ujao, hususani Simba, Yanga na Azam fc.
Afisa
habari wa klabu hiyo Masau Bwire ameuambia mtandao wa MATUKIO DUNIANI kuwa
msimu ujao wa ligi kuu hakuna kulala, watapambana kufa na kupona
kuhakikisha wanapata nafasi tatu za juu.
Masau
alisema katika kuhakikisha wanafanikisha doto yao wameendelea kufanya
vizuri katika usajili na mpaka sasa wamepata nyota watano.
Mchezaji
Juma Seif Dion ‘Kijiko’, aliyekuwa akiichezea Africon Lyon msimu
uliyopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara naye amejiunga na Ruvu Shooting ya
Pwani kwa mkataba wa miaka miwili.
Kijiko
aliyewahi pia kukipiga Yanga, alisaini mkataba huo hivi karibuni
katika ofisi za timu hiyo Mlandizi, Kibaha tayari kuitumikia kwa msimu
ujao.
Kijiko
ni mchezaji wa tano kusaini mkataba na timu hiyo kwa ajili ya msimu
mpya wa ligi, wengine waliosaini ni Ciosmas Ader (Azam), Elias Maguli
(Prison), Juma Nade (Kagera Sugar) na Lambale Jerome (Ashanti).
Wakati
huo huo, uongozi wa timu hiyo ya Ruvu Shooting umetangaza kuwaacha
wachezaji watano kutokana na kiwango chao cha kucheza mpira kushuka.
Ofisa
Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, aliwataja wachezaji hao kua ni
Pail Ndauka, Charles Nobart, Gido Chawala, Frank Mabande na Liberatus
Manyasi.
Kwa
mujibu wa Bwire, timu hiyo tayari iko kambini kikosi cha Jeshi 832 Ruvu
JKT, itaanza mazoezi rasmi siku ya Jumatatu, Juni 24 chini ya Kocha
Mkuu, Charles Mkwasa.
Bwire
amewataka wachezaji wote ambao kawajaripoti kambini wafike haraka kabla
ya Jumatatu ikiwa ni pamoja na wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.
0 comments:
Post a Comment