Mkurugenzi
wa Stoppers Entertainment, Mukhsin Mambo (Mc Stopper) akimvisha Sash
Mrembo Rosemary Peter kuwa Redds Miss Nyamagana 2013
Mkurugenzi
wa Club Fusion wadhamini wa shindano la Miss Nyamagana 2013, Mr. George
akipeana mkono na Redds Miss Nyamagana 2013 Rosemary Peter, mara baada
ya kuvishwa taji
Redds
Miss Nyamagana 2013/14 Rosemary Peter katika pozz, mara baada ya
kutawazwa rasmi kushika taji hilo, katika hafla fupi iliyofanyika katika
hotel ya New Mwanza ya kumvua aliyekuwa akishikila taji hilo Mrembo
Diana Amimo baada ya kudanganya Urai wake na Umri.
Rosemary
Peter, ni mshindi wa pili katika shindano la kumtafuta Redds Miss
Nyamagana 2013, shindano lililofanyika tarehe 11/05/2013 katika ukumbi
wa JB Belmont Hotel jijini Mwanza.Alhamisi
ya tarehe 06/06/2013, Rosemary peter amevishwa taji la Redds Miss
Nyamagana 2013, baada ya Diana Amimo aliyekuwa mshindi wa taji hilo
kudaganya Uraia na umri wake katika shindano hilo.
Udanganyifu
huo uligunduliwa na kuthibitishwa na idara ya uhamiaji mkoa wa Mwanza,
baada ya maafisa wake kumshikilia na kumuhoji mrembo huyo, wiki moja
mara baada ya shindano hilo.
Kwa
Mujibu wa kanuni na vigezo vya mashindano ya urembo hapa nchini, kuwa
Msichana lazima awe raia wa Tanzania na mwenye umri wa miaka 18 hadi 24,
Kampuni ya Stoppers Entertainment, imeweza kumvua taji mrembo Diana
Amimo na kumvisha mshindi wa Pili Rosemary Peter kuwa Redds Miss
Nyamagana 2013/14
0 comments:
Post a Comment