Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Meneja
wa washika bunduki wa jijini London, klabu ya Arsenal, Mfaransa Arsene
Wenger ameendelea kusisitiza nia yake ya kumsajili nyota wa Manchester
United na timu ya taifa ya England Wayne Rooney katika usajili wa majira
ya joto mwaka huu.
Nyota
huyo ambaye usiku wa jana alitumbukiza kimiana bao safi na kuipa timu
yake ya taifa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Brazil, ameonekana kuhitaji
kuihama klabu ya Manchester United msimu ujao wa ligi barani ulaya.
Mwezi uliopita MATUKIO DUNIANI
kupitia mtandao wa kimichezo wa Sportsmail.com ilitoa taarifa kuwa The
Gunners wanataka kuvunja benki na kumsajili Rooney huku wakitangaza
mshahara mnono wa pauni laki mbili na nusu na kumfanya nyota huyo
kulipwa mkwanja mrefu kuliko wote Emirates.
Leo hii mzee Wenger bado ameendeleza kutangaza nia yake hiyo ya kumsajili Rooney mwenye umri wa miaka 27 sasa.
“Rooney ni mchezaji anayemvutia kila mtu duniani, nani anaweza kukataa hilo?” . Wenger ameimbia Televisheni ya Al Jazeera.
Wenger
aliongeza kuwa Changamoto ya kwanza kwa kocha mpya wa United, David
Moyes ni kuvunja tofauti za Rooney na United kama anataka kumbakisha,
vinginevyo lazima atua katika rada zake.
Mbali
na Rooney, Wenger anatamani kumrejesha nahodha wake wa zamani Cesc
Fabregas ambaye hana namba katika kikosi cha kwanza cha Barcelona,
wakati huo huo David Moyes wa United naye alitangaza kuitaka saini ya
Mhispania huyo ili kuziba pengo la Mkongwe Paul Scholes.
Anamuumiza kichwa Wenger: Jembe la United, Wayne Rooney anasemekana anataka kuihama timu yake ya sasa na kunagalia maisha mapya.
Bonge
la Goli: Rooney alifunga bao kali sana katika mchezo wa jana na kuipa
sare ya mabao 2-2 timu yake ya taifa ya England dhidi ya wazee wa Samba,
timu ya taifa ya Brazil katika dimba la Maracana.
Soka
amani tu: Rooney akisalimiani na beki wa timu ya taifa ya Brazil na
klabu ya Barcelona ya Hispania, Dani Alves baada ya mechi yao katika
uwanja wa Maracana
Fulu
mzuka: Rooney alicheza na Alex Oxlade-Chamberlain kuipa sare ya mabao
2-2 England, sasa wanaweza kucheza timu moja kama Arsenal wataweza
kumwaga kitia cha kutosha
Hajatulia
Barca: Cesc Fabregas aliondoka Arsenal mwaka 2011 na kujiunga na Barca,
sasa hana namba katika kikosi cha kwanza na inasemekana anataka kurudi
Emirates kwa mara nyingine tena
Mlezi kwa kweli: Arsene Wenger (kulia) alimkuza kijana mwenye kipaji kikubwa Fabregas na kuwa mchezaji nyota zaidi duniani
0 comments:
Post a Comment